Rais Dk. Jakaya Kikwete amezitaka benki zote nchini kubuni njia
zitakazosaidia kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa vijijini.
Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa kadi yake mpya
ya TPB Popote na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi
(kushoto) kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam
Aliitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya ‘TPB Popote’ iliyobuniwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB).
Rais Kikwete alisema idadi ya mabenki yanayoendesha shughuli zake nchini ni zaidi ya 50, lakini bado matawi mengi yako mijini wakati wananchi walio wengi wako vijijini na nje ya miji.
“Mimi binafsi pamoja na Serikali yetu tumekuwa mstari wa mbele kuona kwamba sekta ya mabenki nchini inatoa msukumo unaotakiwa katika shughuli za kiuchumi nchini, na hasa katika kuwawezesha wazalishaji kuboresha ufanisi na tija, mambo ambayo ni msingi wa ukuaji wa haraka wa uchumi,” alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi wa TPB, Profesa Lettice Rutashobya, alisema ni matarajio yao kwamba, serikali itaendelea kuwasaidia pamoja na mambo mengine, katika mchakato wa kuwaongezea mtaji.
No comments:
Post a Comment