KLABU ya Liverpool imekubali kwamba
inaweza kuumuza mshambuliaji wa kiuruguay Luis Suarez endapo tu timu
inayomtaka italipa kiasi cha paundi millioni 50 - ambayo ndio thamani ya
mshambuliaji huyo kwa mujibu wa Liverpool wenyewe. (HM)
Juzi usiku klabu ya Arsenal ilivunja
bank na kuamua kutoa ofa ya £40million kwa
Liverpool kwa ajili ya
kumsaini Luis Suarez lakini majogoo wa jiji wakaipiga chini ofa hiyo na
kusisitiza kwamba ikiwa Arsenal wanahitaji saini ya Suarez basi inabidi
walipe fedha ambayo ni thamani ya kweli ya mshambuliaji ambayo inatajwa
kuwa £50m - kwa mujibu wa kocha wa Liverpool Brendan Rogers.
"Ikiwa Arsenal wanamtaka Suarez, then inabidi walipe fedha ambayo inaendana na thamani ya kweli ya mchezaji."
Lakini huku Rogers akisema hivyo
imeripotiwa kwamba Arsenal wanataka mshambuliaji mwenyewe alazimishe
kuondoka na kujiunga nao.Arsenal wanaamini kwamba Suarez ameshaamua kwa
dhati kuondoka Anfield ili ajiunge na timu inayocheza soka la ligi ya
mabingwa wa ulaya.
Na wanaamini ofa yao ya £40m imefikia
fedha ambayo inatakiwa kuvunja mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 26 - kitu ambacho kinawapa ruhusa ya kuongea na mchezaji huyo.
Lakini tatizo kubwa kwa Arsenal ni
kwamba wanaamini mshambuliaji huyo angependelea zaidi kujiunga na Real
Madrid ambayo nayo imeomnyesha nia ya kumhitaji.
Real Madrid jana walimuuza
mshambuliaji wao Gonzalo Higuain kwenda Napoli kwa ada ya uhamisho wa
£32 +nyongeza, na hivyo wanaweza kuja kumalizana na Liverpool muda
wowote ikiwa wataachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale ambaye
anaweza kuwagharimu kiasi kisichopungua £70m. Chanzo: shaffihdauda
No comments:
Post a Comment