(PICHA ZOTE NA REUTERS)
TRENI ya abiria imeua takribani watu 78 na
kujeruhi zaidi ya 140 nchini Hispania jana usiku. Katika video
iliyochukuliwa na kamera za CCTV yenye sekunde 11 inaonyesha treni hiyo
ikijaribu kukata kona eneo la Santiago de Compostela, Galicia Kaskazini -
Magharibi mwa Hispania katika spidi kali. Lakini kabla hata haijamaliza
kona hiyo, ilipata ajali mbaya kuanzia mabehewa ya mbele na kusababisha
maafa hayo makubwa. Ajali hiyo imetajwa kuwa miongoni mwa ajali mbaya
za treni kuwahi kutokea balani Ulaya.
Tukio hilo baada ya kunaswa na kamera hizo liliwekwa katika tovuti ya
gazeti la nchini humo la El Pais na baadaye kuwekwa katika tovuti ya
YouTube.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, dereva wa treni yupo katika uchunguzi baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, dereva wa treni yupo katika uchunguzi baada ya tukio hilo.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mariano Rajo, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment