Habari na GAZETI LA MTANZANIA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, ameibua
mjadala ambao tunaona hauwezi kupita hivi hivi bila kuujadili. Spika
Makinda amekuwa mmoja wa viongozi wakubwa wa taifa hili, ambao kila
kukicha wanaibua mijadala mingine ambayo haina tija hata kidogo
kulingana na wadhifa wake.
Juzi, Spika Makinda ameibua mjadala ambao alidai kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakihongwa na Kambi ya Upinzani Bungeni, ili waandike habari zao kwa wingi, kuliko wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa maneno yake bila haya, Spika Makinda anasema waandishi wamekuwa wakipewa ‘kitu kidogo’ (rushwa) katika mikutano ya Bunge inapofanyika mjini Dodoma.
Tumeshangazwa mno na Spika Makinda kutoa maneno haya, ambayo tunaamini akibanwa vizuri atoe ushahidi atabaki mdomo wazi.
Kwa kipindi kirefu tangu akabidhiwe kiti hicho, Spika Makinda amekuwa kiongozi mwenye kauli za kusikitisha mara nyingi na kutuhumiwa kukalia hoja nzito nzito zinazoelekezwa serikalini.
Pia amekuwa akilalamikiwa mno kuwakandamiza wabunge wa upinzani na hata wananchi wa kawaida tu wamekuwa wakijiuliza namna Spika Makinda anavyoendesha mhimili huo.
Hakuna ubishi kwa nyakati tofauti, Spika Makinda amekuwa akilalamikiwa kuwapendelea zaidi wabunge wa CCM katika mambo mengi.
Lakini si nia yetu kueleza mambo mengi, lakini tunataka Spika aueleze umma ni namna gani anavyopotosha jamii juu ya mhimili wa vyombo vya habari.

Tunamtaka
ajitokeze hadharani na atoe ushahidi hadharani ambao unaonyesha Kambi
ya Upinzani Bungeni, imekuwa ikiwahonga waandishi wa habari.
Sisi MTANZANIA, tunamtaka Spika Makinda ajitokeze hadharani na kuviomba radhi, kwani asipofanya hivyo, atakuwa amejipaka matope.
Tunasisitiza kama hatafanya hivyo, ipo siku atajikuta waandishi wanaweka chini kalamu zao na kuacha kuandika habari muhimu za Bunge ambazo wananchi wanapaswa kuzipata wakati wa vikao vya Bunge.
Tunamalizia kwa kuhoji, hivi Spika Makinda hana washauri katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa? Ndiyo maana tunasema tunamshangaa Spika Makinda.
CHANZO CHA HABARI NI GAZETI LA MTANZANIA
No comments:
Post a Comment