MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty
Lulu’ amesema yeye na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki
historia na kamwe hawawezi kurudiana.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema
ameshaamua kutulia na mpenzi wake wa sasa (hakumtaja jina), hivyo hata
iweje hawezi kurudiana na Bond.
“Jamani kwa sasa mnaona nimebadili
kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond atabaki kuwa rafiki kama
walivyo marafiki zangu wengine.
“Niliwahi kuachana naye kipindi
f’lani baadaye tukarudiana lakini hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe
siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu.
AUNTY LULU Mimi niko Tayari kuwa wako wa maisha je upo tayari wewe? waonaje ombi langu kwako?Email yangu hio halindintwari@yahoo.com
ReplyDelete