NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa
kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake,
Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe,
Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea
nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na
Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua
kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.
“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona
filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka
kusema ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema
Uwoya kwa hasira.
Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu
mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza
filamu na Lucy.
“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha
kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo
atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe
hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.
“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.
Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.

No comments:
Post a Comment