Msanii wa filamu Elizabeth Michael
(Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote
alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya
“Foolish Age”.Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe
pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo
muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya
“Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii wa filamu Elizabeth Michael
(Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania
Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu
yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.
Bodi ya
ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya
Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael
‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika
filamu hiyo....
Filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni
nguo fupi zilizotumiwa na waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo
ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama
itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni,
Kwa mujibu wa Lulu Michael,
juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda
na ratiba kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment