CD zinazomuonesha mfanyabiashara mmoja mjini Moshi akifanya ngono zinauzwa kama njugu mjini hapa, Risasi Jumamosi limegundua.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa CD hizo zimekuwa zikiuzwa kwa
wingi maeneo ya stendi ya mabasi ambapo awali moja bei yake ni shilingi
kati ya 4,000 na 5,000 lakini sasa zimepanda na kufikia shilingi 50,000
kutokana na watu wengi kuhitaji.
Sehemu nyingine ambayo mwandishi
wetu alibaini kuuzwa CD hizo za ngono ni sokoni pamoja na kwenye viwanja
vya mpira ambako vijana wamekuwa wakichangamkia kununua.
Video
hiyo inadaiwa kuibwa na mtu asiyejulikana kutoka kwenye kompyuta
mpakato (Laptop) ya mfanyabaishara huyo na haijajulikana ni nani
aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Robert Boaz, amesema mtuhumiwa wa sakata
hilo la CD ya ngono ni kijana mmoja ambaye anamiliki maduka ya kuuza
na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi na
tayari amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA), akitokea Dubai.
“Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha
zilizosambaa kwenye mitandao pamoja na simu kwenye whatsapp ambazo
zinaonyesha watu wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni
kosa la jinai mwanamke kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha
maumbile ama mwanaume amuingilie kinyume na maumbile,” alisema Kamanda
Boaz.
Aliongeza kuwa bado uchunguzi wa picha hizo unaendelea ikiwa
ni pamoja na kumhoji mhusika na kwamba endapo uchunguzi utakamilika
atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha
maumbile kinyume na kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu; kimeweka
adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya
mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Inadaiwa kuwa
mfanyabiashara huyo kijana alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi
wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta ambazo moja kati ya
vipande hivyo inaonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo.
Katika
hatua nyingine, taarifa mbalimbali kutoka eneo la stendi kuu ya mabasi
zinasema baadhi ya wasichana wanaodaiwa kufanya mapenzi na kijana huyo
wameingiwa na hofu kutokana na kuwa na wasiwasi kuwa huwenda kuna video
nyingine ambazo zinadaiwa kurekodiwa na kijana huyo akifanya mapenzi
nao.
“Hapa stendi sasa hivi mabinti waliotembea na jamaa wako roho
juu maana wamekuwa na wasiwasi kuwa inawezekana mshikaji aliwarekodi
kila msichana aliyetembea naye, sasa wana hofu kwani alichofanyiwa
mwenzao kimewatia mashaka,” alisema kijana mmoja muuzaji wa duka la CD
ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini
CREDIT: GLP
No comments:
Post a Comment