MSANII wa Bongo fleva na mshindi wa BSS mwaka jana, Walter
Chilambo, amemshangaa mwenzake Nay Wamitego kuazisha malumbano ya
kijinga dhidi yake ili kujipatia umaarufu.
Chilambo aliyasema hayo jana alipozungumza akisema
msanii huyo amekuwa na fikra finyu kuwa mafanikio ni kumiliki gari.
“Jamaa amezungumza vitu asivyovijua, amekurupuka pasipo kujua na
kwanza hajavifiria kichwani na kuwa mwanamuziki sio lazima kuwa awe na
gari,” alisema Chilambo.
Chilambo ametoa ushauri wa bure kwa msanii mwenzake kusugua kichwa
kwani kuna vingi vya kuimba badala ya kuishia kuwaimba watu moja kwa
moja kwani huo sio usanii.
“Kuna vitu vingi vya kuimba vinavyoweza kuwa na tija kwa taifa, badala
ya kuimba majungu, naamini Nay hayajui kwa undani maisha yangu, hajua
hata ninapoishi,” alisema.
Alipoulizwa kama anafikiria kumshtaki au kumjibu kwa wimbo, Chilambo alisema yote mawili hayana tija kwake wala kwa muziki.
‘Mimi siko kiushindani zaidi, nawaza kutoa wimbo ambao utawagusa
mashabiki wangu ili nami nipate fedha badala ya kazi ya majungu,”
alisema Chilambo.
Alipofuatwa Mkurugenzi wa Bechmark Production Ltd, Madam Ritha
Poulsen, aliyetajwa kwenye wimbo huo kuashiria kuna yaliyojificha nyuma
ya zawadi za washindi, alisema hakuna hila wala agenda ya siri kwenye
suala la zawadi.
‘Mimi sina ajenda ya siri. Namtakia kila la heri, naamini yeye (Nay)
ni mhangaikaji, anayejaribu kutumia jina letu kutoka,” alisema Ritha.
Majibu ya Rita ni baada ya Nay kuwashutumu kupitia wimbo akidai
waandaji wa BSS wana ajenda ya siri, baada ya msanii waliyemuibua kuishi
maisha ya ufukara akiwa hana hata gari wala baiskeli.
No comments:
Post a Comment