Mapema wiki hii Msomali mwenye asili ya Kenya Abdi Guyo alijitokeza na
kudai kuwa yeye ndiye baba halisi wa mshindi wa BBA the Chase
Dillish,akisema alimpata binti huyo huko Namibia 1989 wakati wa mpango
wa kuleta amani nchini humo.
Dillish na Abdi ambaye imethibitishwa ni baba yake |
Habari hiyo ilipotoka mwanadada Dillish hakukubaliana nayo kiasi cha
kwenda kwenye mtandao wa kijamii wa twitter akishangaa kuwa huyo ni baba
yake akaenda mbali zaidi akiuliza kwa kebehi kuwa baba yake ni Msomali.
Hazikupita saa nyingi sasa mama wa Dillish anayeitwa Selma amethibitisha kuwa mwanaume huyo anayeitwa ABDI ndio baba halisi wa Dillish.
Kwenye shughuli ya Google hangout iliyandaliwa na ubalozi wa Kenya nchini Namibia,Selma na Abdi waliruhusiwa kuzungumza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23.Selma aliungana na balozi wa Kenya nchini Namibia Peter Gitau,Mjomba wa Dillish na shangazi yake.Abdi akafafanua kuwa amekuwa akitaka kufanya mawasiliano ya karibu zaidi lakini ratiba ya jeshi ilikuwa moja ya vikwazo na ikikwamisha mawasiliano hayo kiasi cha kutokea kutengana kwa muda na akakana kujitokeza kwa sababu ya mkwanja aliopata Dillish baada ya kushinda..
Mwisho wa shughuli hiyo baba huyo wa Dillish,Abdi akaalikwa kwenye sherehe za kuzaliwa Dillish itayofanyika September 16 atapotimiza miaka 23.
Hatimaye sasa Dillish anamfahamu baba yake ambaye ni raia wa Kenya,swali la kujiuliza ni je kwakuwa baba halisi wa Dillish ni raia wa Kenya,tunaweza kusema Kenya imeshinda shindano la BBA The chase na si Namibia? Lakini kwa nini baba huyo hakujitokeza kabla ya Dillish kupata ushindi? Au ndio kaona mkwanja tena hehe! Tafakari.
No comments:
Post a Comment