Dar es Salaam.
Wakati baadhi ya wagombea walioenguliwa kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakijiandaa kukata rufaa, mgombea mwingine Richard Rukambura amesema atakwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi huo mpaka kesi yake ya kupinga kuenguliwa itakaposikilizwa.
Wakati baadhi ya wagombea walioenguliwa kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakijiandaa kukata rufaa, mgombea mwingine Richard Rukambura amesema atakwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi huo mpaka kesi yake ya kupinga kuenguliwa itakaposikilizwa.
Kamati ya Uchaguzi TFF, imepitisha majina ya wagombea 40 kati ya 58 kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utakaofanyika baadaye mwezi ujao.
Wakizungumza na gazeti hil jana, wagombea Shaffih
Dauda, Ayubu Nyenzi, Eliud Mvela na Samwel Nyala wamesema hawakubaliani
na uamuzi uliofikiwa dhidi yao, hivyo wanakwenda Kamati ya Rufaa TFF
kupinga kutoswa.
Nyalla alisema anatarajia kuwasilisha rufaa yake wakati wowote kupinga kuenguliwa kwake, akiamini uamuzi huo hakuwa sahihi kwa vile ana sifa zote za kuwania nafasi ya Mjumbe Kamati ya Utendaji.
“Nadhani busara itatumika kunipa haki yangu. Mimi ni raia wa Tanzania, elimu ninayo na mambo mengine mengi, sasa kwa nini nimeenguliwa,” alisema Nyala.
Samwel Nyalla ameondolewa kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi wa TFF kwa kutoonesha malengo yake.
Kwa upande wake Shaffih alisema: “Sikubali, nitakata rufaa. Mimi ni mwandishi wa habari, nina vyanzo vingi vya kupata habari. Sasa hiyo isiwe sababu ya kuninyima haki yangu ya kugombea.
Eliud Mvela alisema anakusanya vielelezo vyake ili akakate rufaa. “Siwezi kukubali kirahisi sababu za kuenguliwa kwangu, ambazo hazina mashiko hata kidogo. Mimi ni raia wa Tanzania.”
Rukambura aliyekuwa akiwania nafasi ya urais,
alisema hajaridhika na kigezo kilichotumika kumuengua na haoni sababu ya
kukata rufaa kwa kulipa Sh1 milioni na kuinufaisha TFF.
“Hata ukikata rufaa leo, uamuzi utakuwa huohuo,
sioni sababu ya kutata rufaa, nakwenda mahakamani,” alisema Rukambura,
ambaye kama jaribio lake la kufungua kesi litafanikiwa, basi itakuwa ni
mara ya pili kufanya hivyo.
Rukambura alikata rufaa kupinga kuenguliwa kwenye uchaguzi wa awali uliokuwa ufanyike Februari 23 mwaka huu kabla ya kusimamishwa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).
No comments:
Post a Comment