Siku ya jana katika interview na baby Madaha ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mnono na kampuni ya Candy n’ Candy Records ya jijini Nairobi nchini Kenya , Bongomovie.com wameweza kupata mambo matano ambayo mashabiki wa mwanadada huyu watakuwa hawajui kumhusu yeye.
Katika interview hiyo, baby Madaha ametaja mambo matano ambayo anasema mashabiki wake wanahitaji kuyafahamu kumhusu yeye. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. I’m single ( Sina mpenzi)
Mwanadada huyu amesema kuwa kwa sasa yupo single na yuko bize na PESA. Ila kama kuna mwanaume mwenye nia ya dhati anaweza kumtafuta.
2. Anasoma degree ya sanaa kwenye sayansi ya siasa na historia (B.A- Political science and History) - chuo kikuu huria jijini Dar es Salaam..
3. Mama yake mzazi ndio rafiki yake mkubwa maishani
4. Ni mpenzi wa soka na ni mshabiki wa Chelsea na anavutiwa na Kevin-Prince Boateng wa club Schalke 04 ambaye ndiye alisababisha akanyoa nywele staili aliyonayo baby madaha kwa sasa.
No comments:
Post a Comment