Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila
Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa
katwa mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa
mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida.
Awila ambaye amelazwa wodi 2 katika hospitali ya mkoa amedai kuwa baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani.
Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi.

No comments:
Post a Comment