Mshambuliaji wa klabu ya AS Roma Gervinho amemsema kocha wake wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kwa kutokuwa na imani na uwezo wake wakati alipokuwa na timu hiyo ya London.
Gervinho, 26, alijiunga na Gunners mwaka 2011 kwa ada ya uhamisho ya £10.8million akitokea Lille,
lakini baada ya kufunga mabao 9 ya ligi katika miaka yake ya miwili, akauzwa kwenda
Serie A.
Lakini pamoja na kuonyesha kiwango kisichovutia katika Premier League, amemlaumu Wenger kwa kumfanya kutojiamini kwa kutompa nafasi kubwa uwanjani.
Akiongea na SunSport, Gervinho alisema: 'Nilikuwa sipewi muda mrefu dimbani na nilikuwa nahitaji ili kuwa bora zaidi na kucheza soka safi.
'Wenger hakuwa tayari kunipa muda wa kuonyesha vizuri uwezo wangu.
'Pia nafasi yangu haikuwa kwenye winga na sikutegemewa hilo na halikunifurahisha kabisa..'

No comments:
Post a Comment