KIGAUNI kifupi alichokitinga mwigizaji Chuchu Hans (pichani)
katika uzinduzi wa filamu ya Lulu kilizua gumzo kwa mashabiki kutokana
na ufupi wake.
Chuchu
alikitinga kigauni hicho hivi karibuni katika Ukumbi wa Mlimani City
ambapo wadau mbalimbali walianza kuibua minong’ono kuwa huenda alipokaa
kwenye kiti, alikalia mwili bila kuwa na nguo.
Baada ya paparazi wetu kupokea minong’ono hiyo kutoka kwa wambea,
fasta alimfotoa picha na kumuuliza kama ni kweli amekalia kiti bila ya
nguo.
“Mh! Jamani Wabongo bwana, sasa hapa tatizo ni nini? Mbona mimi naona kawaida tu, tatizo lipo wapi?” alihoji Chuchu
No comments:
Post a Comment