Malumbano makali yametokea ndani ya ukumbi wa bunge kwa mara ya pili tangu kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013 kwa kile kinachodaiwa Muswada huo una mapungufu na haukuwashirikisha ipasavyo wananchi wa Zanzibar
Malumbano hayo yalipeleke Kiongozi wa Kambi rasmi kutolewa nje na Askari wa Bunge baada ya Muongozo kutoka kambi ya upinzani kumtaka Naibu Spika Kuahirisha Bunge mpaka Muswada huo utakapofanyiwa marekebisho.
Hali hii imetokea baada ya hoja kutolewa na mh Ally Seif Mbunge kutoka Chama cha Wananchi CUF kulitaka Bunge lisitishe Shughuli zake ili Kamati iende Zanzibar kupata Maoni upya. Baada ya muongozo huo Naibu Spika anatoa ufafanuzi.
Insert- Job Ndugai Naibu Spika
Insert- Job Ndugai Naibu Spika
Bado hali ikawa tete pale Mh Tundu Lissu Msemaji Mkuu Wizara sheria na katiba akasimama na kumtupia lawama wenyekiti wa Kamati ya Kudumu Katiba Sheria na Utawala
Ni Baada ya ufafanuzi huo wa serikali Bunge linaamua kupiga kura ili Majadiliano ya Muswada huo Muhimu kwa Watanzania uendelee lakini njia ya kupiga kura haikufua dafu baada ya Wabunge wa upinzani kuzuia kiongozi wa kambi hiyo asiotolewe nje ya ukumbi wa bunge
Hatimaye Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje na Bunge likaendelea na Mjadala wa Muswada wa Sheria wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment