Mbio za mwenge zilipiga kambi katika wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar hapo jana Septemba 08,
ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (hayupo
pichani)na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sofia Mgema
walihudhuria mapokezi hayo.
Pia
viongozi mbalimbali wa serikali, watumishi wa umma na wananchi kutoka
sehemu tofauti hapa jijini Dar waliokuwepo kwa pamoja waliupokea Mwenge
huo na kushiriki michezo iliyoandaliwa kwa niaba ya kiongozi wa mbio za
Mwenge kwa mwaka huu, Juma Ali Simwai. Kauli mbiu ikiwa ni:
“Watanzania ni wamoja tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini,
itikadi, rangi na rasilimali.”
Mkuu wa Wilaya ya Temeke akikabidhi Mwenge kwa Kiongozio wa Mbio za Mwenge, Juma Ali SimwaiJuma Ali Simwai (kushoto) akiwa ameketi sehemu aliyoandaliwa , kushoto ni wenyeji wake.Mkuu wa Wilaya ya Temeke akikabidhi Risala kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Juma Ali Simwai akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sofia Mgema mara baada ya kukabidhiwa Risala.
(PICHA NA CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA/ GPL)
No comments:
Post a Comment