MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sofia
Simba, ameizidi kete kambi ya mpinzani wake, Mama Anna Kilango Malecela.
Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto ameizidi kete kambi ya Mama Kilango ambao waligomea uteuzi wa
manaibu makatibu wakuu Bara na Visiwani, uliofanywa na Simba.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zilisema kuwa baada
ya kugomewa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Taifa ya Jumuiya ya
Wanawake wa CCM (UWT) na kusababisha kikao kuvunjika, Waziri Simba sasa
amefanikiwa kupitisha majina hayo na wateule hao sasa wameanza kazi.
Habari zinasema kuwa wajumbe wa kikao hicho ambao baadhi wanadaiwa
kuwa ni wafuasi wa Mama Kilango waliopambana kwenye uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo taifa, waligomea uteuzi wa majina hayo kwa
madai kuwa hawana sifa.
“Baada ya kugomewa, mwenyekiti aliwazidi kete kwa kwenda kwa rais na
kumueleza sababu za uteuzi wa majina hayo na sasa watendaji wao wako
ofisini,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Wakati wa uchaguzi wa UWT, Waziri Simba ambaye alikuwa akitetea nafasi
hiyo, alichuana vikali na Mama Kilango huku kila kambi ikidai kuchezewa
rafu.
Katika kikao hicho kilichofanyika mwezi uliopita kwenye Makao Makuu ya
Jumuiya hiyo jijini Dare es Salaam na kuvunjika, Mama Simba
aliwasilisha jina la Salama Aboud Talib kutoka Zanzibar na Ever Kiwele
wa Bara.
Vurugu kubwa zimetokea katika kikao cha utezi wa majina ya viongozi
hao na kusababisha kuvunjika baada ya wajumbe kupinga uteuzi huo kwa
madai kuwa hawana sifa.
Chanzo cha kuvunjika kwa kikao hicho ni vuta ni kuvute ya nani ateuliwe kushika wadhifa wa Naibu Katibu Bara na Zanzibar.Chanzo Tanzania Daima.
No comments:
Post a Comment