EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 15, 2013

Mwakyembe awashukia vigogo wa Bandari Dar

Dar es Salaam. 
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameipa siku moja Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kutaja majina ya watu wanaoiba mafuta katika bomba kubwa la kupakulia mafuta bandarini (SBM).
 
Alisema wezi hao bila woga wowote wametoboa bomba hilo ambalo ujenzi wake umeigharimu serikali mamilioni ya fedha, kuunganisha mabomba yao chini kwa chini kisha kunyonya mafuta hadi kwenye vituo vyao vya kuhifadhia mafuta.

“Haiwezekani wizi huo ukafanyika bila TPA kuwajua wahusika kwa sababu hujuma hii inaonyesha kuwa inafanywa na watu wenye utaalamu wa hali ya juu,” alisema Dk Mwakyembe jana wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu changamoto na mafaniko katika utendaji wao wa kazi.

Alisema wezi hao wamekuwa wakiibia serikali lita 35,000 hadi 40,000 za mafuta katika kipindi kisichojulikana. Ujenzi wa bomba hilo ulikamilika takriban mwaka mmoja uliopita.

Alisisitiza, “Wizi umepungua kwa kiasi kikubwa TPA katika hilo nawapongeza, lakini wapo wachache ambao siyo waaminifu wamebuni mbinu mpya za kuihujumu serikali. Nataka mpaka Jumatatu (kesho) saa 6 mchana niwe nimeletewa hayo majina.”

Alisema wizi huo unafanyika katika Kampuni ya kuhifadhia mafuta ya Tipper, huku akiagiza kampuni hiyo kuvunja mkataba na kampuni ya ulinzi inayolinda mafuta hayo.

“Hao Tipper nao inatakiwa muwalete ili wawataje waliohusika na wizi huo. Pia nasikia kuna raia mmoja wa kigeni (mzungu) anatoa rushwa ili kufanikisha wizi huu. Katika hili nasema watarudi kwao Ulaya,” alisema na kuongeza:

“Suala hili nimeshamfikishia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu uhujumu uchumi unaofanywa na kampuni hii ya Tipper, amesikitika kweli.”
Alisema kutokana na uzito wa suala hilo anashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini ili kuhakikisha kuwa wote waliohusika wanachukuliwa hatua.

“Serikali haitakaa kimya katika hili, kilichofanyika ni hujuma ambayo ingeweza kuangusha uchumi wa nchi na kuzorotesha huduma za kijamii. Ni lazima wahusika washughulikiwe” alisema.

Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe aliutaka uongozi wa TPA kuachana na mpango wake wa kupeleka boti na mitambo mingine kwenye karakana zilizoko Mombasa, Kenya, kwa ajili ya matengenezo, “Huu mpango ni wa ulaji wa wachache tu.”
Alisema mamlaka hiyo inatakiwa kujipanga kwa kuandaa bajeti itakayowasaidia kujenga karakana yake

Aishukia bodi
Katika mkutano huo, alisema bodi ya TPA ina ufa na kusisitiza kuwa mambo mengi yanayotokea ndani ya mamlaka hiyo yanasababishwa na baadhi ya vigogo kugombea ulaji kitendo ambacho kinawakatisha tamaa wafanyakazi wa chini.
“Nimeshagundua ufa huu labda niwaambie kitu, mimi nina saruji ya kuuziba huu ufa,” alisisitiza.

Kuhusu wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Dk Mwakyembe ameutaka uongozi wa TPA kuhakikisha unasimamia haki za wafanyakazi wote bila ubaguzi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate