Amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na anaendelea vyema na matibabu.
Mwandishi wa Habari wa kujitegemea mkoani Singida wa Magazeti ya Mwananchi Communications Limited, Awila Silla akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, baada ya kupigwa mapanga na mtu asiyejulikana Jumapili iliyopita, mwaka huu, mjini Singida.
Singida.
Mwandishi wa Habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti mkoani Singida, Awila Silla amejeruhiwa baada ya kukatwa na mapanga kichwani na mtu asiyejulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku Jumapili iliyopita maeneo ya Utemini ambapo alivamiwa na mtu huyo ambao mbali na kumjeruhi kwa mapanga, pia alimpiga ngumi na mateke na kumjeruhi katika jicho lake la kushoto.
Silla amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida
ambapo alifikishwa na kijana mmoja (jina halikumbuki) ambaye alimkuta
akiwa hajitambui.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hana taarifa yoyote na kuahidi kuwa atafuatilia tukio hilo.
Tangu afikishwe katika hospitali hiyo, watu
mbalimbali walikwenda kumjulia hali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone.
Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini, Silla
alisema, nilikuwa nikirejea nyumbani muda ya jioni nilipofika maeneo ya
Utemini simu yake ya kiganjani ikaita na kulazimika kuzungumza ghafla
akatokea kijana ambaye alikuwa amejifunika shuka la kimasai na kuanza
kumfuata.
“Nilipogundua yule kijana ananifuata kwa kasi nikaongeza mwendo lakini kila nilipojaribu kumkwepa alizidi kunifuata mpaka nilipofika karibu na uzio wa nyumba moja akanikaribia na kuanza kunivamia kisha kunibamiza katika geti la nyumba hiyo.”
Alisema baada ya kufanikiwa kunidhibiti akaanza
kunicharanga na mapanga huku akidai nimpatie pesa, nikamwambia sina pesa
lakini cha kushangaza akasema wewe huwa una hela.
“Alinishangaza sana, inaonekana kama ananijua, lakini kila nilipokuwa namkaribia ili nimjue vizuri alikuwa anazidi kunisukuma nisimgundue.”
Kwa mujibu wa Silla, mtu huyo alimnyang’anya simu
pamoja na mfuko uliokuwa na vifaa vidogo ambavyo alitoka kununua
yakiwamo mafuta.
No comments:
Post a Comment