MAITI ya mwanamke aliyeripotiwa kuchinjwa kikatili na mwanaume
aliyesadikika kuwa ni mume wake, Yusta Ernest (28), ameagwa kwa majonzi
makubwa kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani kwa mazishi.
Tukio hilo la kuagwa lilifanyika mapema leo hii katika Hospitali ya
Mwananyamala jijini Dar, na kuibua upya majonzi makubwa kwa ndugu na
marafiki wa marehemu ambao wengi walionyesha wazi hisia zao kuwa
wameumizwa na kifo cha kipenzi chao.
Akiongea kwa majonzi msemaji wa
familia hiyo, Nelson Mgerwa alisema kuwa familia imeumizwa sana na kifo
cha ndugu yao mpendwa ambaye ameondoka akiwa na umri mdogo.
Mwili
wa marehemu umesafirishwa leo kuelekea Mpwapwa mkoani Dodoma, ambapo
taratibu zote za mazishi zitafanyika katika kijiji cha Nzasa mkoani
humo.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)
No comments:
Post a Comment