Moshi mkubwa ukitoka katika meli hiyo baada ya wahusika kujitosa majini.MV Gold Star ikipelekwa katika Bandari ya Sicilia.
-NI MV GOLD STAR -WATUHUMIWA WAICHOMA MOTO KUPOTEZA USHAHIDI, WAJITOSA MAJINI -ILIKUWA NA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA BILIONI 126.5 -MZIGO ULIOKUWEMO NI TANI 30 ZILIZOKUWA ZINAPELEKWA UTURUKI -9 WAKAMATWA, NI RAIA WA MISRI NA SYRIA
MELI iliyosajiliwa nchini Tanzania ya MV Gold Star juzi Ijumaa
imekamatwa nchini Italia ikiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni
milioni 50 sawa na shilingi bilioni 126. 5.
Watuhumiwa waliokuwa ndani
ya meli hiyo waliamua kuichoma moto ili kupoteza ushahidi na kuamua
kupiga mbizi majini lakini walitiwa nguvuni na wanausalama wa Italia.
Meli hiyo ya mizigo ilikuwa imepakia tani 30 za madawa na ilikamatwa
jirani na Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini
Italia wakati ikielekea Uturuki. Maofisa wa polisi nchini humo wamedai
kuwa watuhumiwa tisa waliokamatwa ni raia wa Misri na Syria na
watafikishwa mbele ya sheria. Moto katika meli hiyo umezimwa na tayari
imepelekwa katika Bandari ya Sicilia.
No comments:
Post a Comment