CHAMA cha
Wananchi (CUF) kimemtaka Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aiombe radhi
Kambi ya Upinzani kwa kitendo cha kumtoa ndani ya Bunge kiongozi wa
kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es
Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro alisema
kitendo hicho ni ukiukaji wa kanuni na sheria za Bunge, na
kimeidhalilisha kambi hiyo.
"Tukio
lililotokea jana (juzi), si la kawaida, Naibu Spika ni kiongozi wa Bunge
lakini wapo watu wakubwa ambao anapaswa kuheshimika sana.
"Kambi ya Upinzani ina kiongozi wake ambaye ni Freeman Mbowe mwenye nafasi kubwa kama aliyonayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
"Tofauti ya Pinda ipo nje ya Bunge wakiwa ndani ya Bunge wote wana heshima ya kufanana.
"Sijui
jeuri ya Ndugai imetoka wapi hivi Pinda angekuwa amesimama Naibu Spika
angewaamuru askari wa Bunge wamtoe? Ndugai anapaswa kuomba radhi kwa
njia ya ustaarabu tu,"alisema Mtatiro.
Naye
Oliver Oswald anaripoti kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus
Kibamba amelishauri Bunge kutumia mfumo wa kupiga kura katika kutafuta
au kutoa uamuzi kuepusha mizozo ya mara kwa mara inayozidi kujitokeza
katika vikao vya bunge mjini Dodoma.
Alisema
inafaa utaratibu huo ukatumika bungeni kurudisha nidhamu iliyopotea kwa
kipindi kirefu kwa sababu mizozo hiyo inazidi kutoa sifa mbaya kwa
wapiga kura na jamii kwa ujumla:CHANZO MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment