Kikosi
cha timu ya Airtel Rising Stars kutoka Tanzania wakati wa ufunguzi wa
michuano ya Airtel Rising Stars ya Afrika iliyozinduliwa rasmi jana
(Jumatatu) nchini Nigeria na kushirikisha timu kutoka katika nchi 17
barani Afrika.
Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel, Bi. Lilian Kibiriti.
Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel, Bi. Lilian Kibiriti.
Kikosi cha timu ya wasichana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. Mwenye suti ni kocha wa timu hiyo, Rogacian Kaijage.
TIMU ZINAZOSHIRIKI MICHUANO YA VIJANA YA AIRTEL RISING STARS ZAWASILI NCHINI NIGERIA
· Michuano hiyo inafanyika Lagos, Nigeria kuanzia Septemba 16 hadi 22, 2013
· Michuano hiyo inafanyika Lagos, Nigeria kuanzia Septemba 16 hadi 22, 2013
TIMU zinazoshiriki michauano ya pili ya
Afrika ya Airtel Rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu,
zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana katika Viwanja vya
Agege. Michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji mahiri wa zamani wakiwemo
Robert Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal.
Timu ya Zambia ilikuwa ya kwanza kutua siku ya Ijumaa ikifuatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo.
Kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya Jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve.
Michuano ya Airtel Rising Stars ni michuano
ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji
huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa kwa
kupitia mashindano haya. Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza
ndoto zao na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu, alisema
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Nigeria, Bwana Segun Ogunsanya
Aliongeza kuwa "Wachezaji wengi wameshiriki
michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata
nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine kutoka katika nchi
mbalimbali. Kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na
kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote."
Michuano ya Airtel Rising Stars itafanyika
jijini Lagos nchini Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 Septemba 2013.
Wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika kliniki
itakayosimamiwa na makocha wa Manchester United inayotegemea kufanyika
Aprili 2014 jijini Lubumbashi, DRC.
No comments:
Post a Comment