Wakati Wanzibari wakiadhimisha miaka miwili tangu kuzama kwa
Meli ya Mv Spice Islanders, imeelezwa kuwa uingiaji na utokaji wa abiria
katika vyombo vya usafiri katika Bandari ya Malindi, si salama.
Hayao yametanabahishwa na washiriki wa kongamano la kumbukumbu ya kuzama kwa meli hiyo.
Ofisa Mwaadamizi wa Kampuni ya Azam Marine,
Abdulrazak Shan Ismail, alisema udhibiti wa abiria wanaoingia na kutoka
katika vyombo vya usafiri katika bandari hiyo, unapaswa kuangaliwa upya.
Abdulrazak alisema kukosekana kwa umakini katika sehumu ya kutokea magari yanayotuimiwa na abiria kuingia na kutoka, kunahataraisha usalama wao. (Mwinyi Sadallah)
No comments:
Post a Comment