Polisi nchini Nigeria wanawasaka wanaume waliomteka
nyara kiongozi wa ngazi ya pili wa kanisa la kianglikana nchini Nigeria
Askofu mkuu Ignatius Kattey.
Askofu Ignatius ni mkuu wa kanisa la kianglikana tawi la jimbo la Niger Delta.
Ignatius Kattey. |
Alitekwa nyara Ijumaa jioni akiwa na mkewe Beatrice, karibu na makao yao mjini Port Harcourt, Kusini mwa nchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, visa vya watu
kuteka nyara wakati wakidai kulipwa kikombozi vimekuwa jambo la kawaida
katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta linalozingira Port
Harcourt
Mwaka jana mamake waziri wa fedha, Ngozi Okonjo-Iweala alitekwa nyara na kuzuiliwa kwa siku tano.
Hakuna kundi lolote limedai kumkamta Askofu huyo akiwa na mkewe.
Makundi mengi ya magenge ya watu waliojihami,
huendesha shughuli zao katika eneo hilo kutokana na miaka mingi ya
migogoro katika eneo hilo dhidi ya sekta ya mafuta.
No comments:
Post a Comment