Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakichukua chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi |
Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi konyagi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi |
NA MWANDISHI WETU
WAREMBO wanaowania taji la Miss Tanzania wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Wito huo umetolewa na
Mkurugenzi mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries (KONYAGI) Bw. David
Mgwassa wakati akiongea na Warembo 30 wanaowani taji la Miss Tanzania
walipotembelea kiwanda hicho jijini Dar es salaam.
"Nyinyi ni mabalozi wazuri
wa kutangaza bidhaa za humu ndani hivyo nawaomba sana mzipende na
kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda vya ndani" alisema
Bw. Mgwassa.
Amesema kuwa TDL kupitia
kinywaji cha Zanzi imeamua kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa kiasi
cha Milioni 40 ikiwa na lengo la kutangaza kinywaji hicho na pia
kuboresha shindano hilo.
Kwa mujibu wa Bw. Mgwassa
shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa taifa hili na kuwataka
warembo hao kutangaza milima kilimanjaro na pia kuitangaza Zanzi kuwa
ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
"Nyinyi warembo naombeni
sana Zanzi iwe kwenye mawazo yenu kila siku na muitangaze Zanzi baada
ya mlima kilimanjaro kwa kufanya hivyo basi uchumi wa nchiu pia utakua
mzuri zaidi." alisema
Kwa upande wake meneja
masoko wa TDL, Bw. Vimal Vaghmaria aliwataka warembo hao kuwa na nidhamu
kubwa wanapokuwa kambini kwa lengo la kupata mrembo mwenye viwango vya
juu na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
"Sisi kama TDL kupitia
kinywaji cha Zanzi tumemua kudhamini shindano hili la Miss Tanzania
tukiamini kuwa nyinyi ni mabalozi wazuri wa kuitangaza kinywaji hichi na
kuiletea sifa Tanzania" alisema Bw. Vaghmaria.
Katika ziara hiyo warembo
walipata nafasi ya kujione shughuli mbalimbali za kiwanda hicho kuanzia
mwanzo wa vinywaji vinapozalishwa hadi kwenye sehemu ya mwisho ya
upakiaji.
No comments:
Post a Comment