Klabu ya Yanga tayari imewasilisha
rufaa yake kwa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kucheza mchezo wake
katika hali isiyokuwa na usalama na kuomba mchezo huo urudiwe katika
uwanja wa ugenini kwa timu zote.
Mchezo hu ambao
ulitawaliwa na vurugu kutoka kwa washabiki wa Mbeya City ulichezeshwa na
mwamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ambaye pia hakutoka maamuzi
sahihi kwa kukataa bao halali la mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya
70 ya mchezo.
Mashabiki wa Mbeya City
walirusha chupa za bia na mawe kwenye bus la timu ya Yanga na kuvunja
kioo cha bus kubwa upande wa dereva na kumjeruhi mkononi hali
iliyoplekea wachezaji wa Yanga kucheza kwa hofu katika mchezo huo
wakihofia usalama wao.
Afisa habari wa Yanga
Baraka Kizuguto aliwasilisha taarifa hizo kwa kamisaa wa mchezo juu ya
matukio hayo na ushahidi wa kipande cha chupa kilichorushwa na kumjeruhi
dereva baada ya kupasua kioo.
Tukio hilo la
kabla ya mchezo lilipelekea timu ya Yanga kucheza kwa woga na wasiwasi
juu ya usalama wao(under protest) kitu ambacho kikanuni kinairuhusu timu
iliyokutwa na matatizo hayo kuka rufaa kuhusiana na hali ya usalama
iliyojitokeza.
Aidha
klabu ya Yanga pia inaomba kuhakikishwa usalama na shirikisho la soka
nchini (TFF) katka mchezo wa siku ya jumatano dhidi ya timu ya Prisons
vinginevyo inaomba mchezo huo pia uhamishiwe katika uwanja wa ugenini
kutokana na kutokua na uhakika wa usalama.
Katika
mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ulimalizika kwa sare ya
bao 1-1, mchezo uliofanyika katika dimba la uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment