HATIMAYE modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Kete zinazosadikiwa kukutwa na modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ akiwa amezimeza.
Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza
tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana
akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia.
“Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema chanzo chetu.
Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.
Jack akiwa karibu na madawa aliyonaswa nayo.
KUNA MADAI ALIZOMEWAChanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment