Msanii wa filamu, Wema Sepetu akiwa na kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, wakiwa katika ofisi za Global Publishers jana.
Na Mwandishi WetuKOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic, jana alikutana na msanii wa filamu, Wema Sepetu na kupiga stori kwa dakika 20.
Logarusic jana alitembelea Ofisini za Championi za jijini Dar es Salaam na wakati akizungumza na baadhi ya wafanyakazi, Wema aliibuka na ndipo wawili hao walipoanza kupiga stori za hapa na pale.
Loga aliwashangaza wengi baada ya kuonyesha kuwa anamfahamu zaidi Wema kwa kuanza kumuuliza kuhusu mambo kadhaa zikiwemo filamu zake.
Hata hivyo, Wema ambaye amekuwa akifuatilia baadhi ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, naye mara moja alionyesha kuwa anamfahamu Loga na kuanza kumhoji kuhusu changamoto anazokutana nazo kwenye timu yake ya Simba.
Baada ya kusimama kwa muda wawili hao walisogea pembeni ambapo walikaa na kuzungumza kwa dakika 20, huku kila mmoja akionyesha kufurahishwa na stori hizo kwani walicheka mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment