Pengo akemea ndoa za mikataba, mashoga
akemea ndoa za mikataba, mashoga
Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Palycarp Kardinali Pengo
amekema ndoa za jinsi moja na zile za mkataba kwa sababu ni kinyume cha
maadili ya dini zote na zinachangia kuharibu familia.
Akizungumza katika sikukuu ya mapadri na kubariki mafuta ya krisma
katika Kanisa la Mtakatifu. Joseph, Dar es Salaam, Pengo alisema ndoa za
mkataba zinachangia kwa kiasi kikubwa wanandoa kutokuwa waaminifu na
kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinazaa familia ambazo hazina
maadili.Kuna wanandoa wanaona kukaa na mwenza wake kwa muda wote ni jambo
ambalo halikubaliki, wanajiingiza katika ndoa za mkataba ili waweze
kufanya matendo mengine ambayo hayampendezi Mungu na hapo ndipo
wanajenga familia isiyokuwa na maadili,¡± alisema.
Kuhusu ushoga, Pengo alisema: ¡°Hatuwezi kuwa na familia imara kama
hatutakemea mazingira haya ya ndoa za jinsi moja na hatuwezi kuzungumzia
uhai wa kuwa na familia bora wakati kuna kikwazo ambacho hakiendani na
maadili ya dini zote.¡
Kardinali Pengo pia aliwaonya mapadri wanaotumia fedha za kanisa kwa
masilahi binafsi akiwataka kuacha tabia hiyo mara moja. Alionya kwamba
endapo watabainika, kanisa halitatoa fedha kulipa faini au fidia
itakayotokana na uzembe huo.
Aliwashukuru waumini wa Dar es Salaam kwa kumpatia zawadi ya Sh43
milioni wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya uaskofu na kuahidi
kuzitumia katika ujenzi wa Shule ya Msingi Kisiwani iliyopo Mafia.
MCL
No comments:
Post a Comment