REAL Madrid imetwaa Kombe la Mfalme baada ya kuichapa Barcelona mabao 2-1 usiku huu Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, Hispania.
Real
walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11, mfungaji Angel di Maria
akimalizia pasi ya Karim Benzema, lakini Bartra akaisawazishia Barca
dakika ya 68 kwa pasi ya Xavi.
Shujaa wa Real hii leo alikuwa na nyota wa Wales, Gareth Bale aliyefunga bao la ushindi dakika ya 85 kwa pasi ya Fabio Coentrao.
|
Wafalme; Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kushoto akishangilia na Alonso kulia |
|
Bingwa Mfalme; Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kulia akipiga shuti pembeni ya Dani Alves |
Mwanasoka
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alikuwa nje leo akiendelea kuugulia
maumivu yake na aliungana na wenzake kuwapongeza baada ya mechi kwa
ushindi huo.
Baada
ya kunyakua taji la kwanza msimu huu, Real sasa inaelekeza nguvu zake
katika mataji mengine mawili, La Liga na Ligi ya Mabingwa ambako imefika
hatua ya Nusu Fainali na itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern
Munich.
Kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, Real inachuana na Atletico Madrid walio kileleni na Barca walio nafasi ya tatu.
Mashabiki wa Real Madrid wakisherehekea taji la Copa del Rey Uwanja wa Mestalla
Lionel Messi akilalamika baada ya kipigo cha Barcelona kwa wapinzani wao, Real Madrid mjini Valencia
|
Ronaldo akitazama mechi leo Mestalla |
Angel di Maria akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Real
Bartra akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona
Gareth Bale akipiga shuti mbele ya Javier Mascherano
No comments:
Post a Comment