Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu zito baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni
wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa
akiandaa filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha
Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
“Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo
yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo
na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na
Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo. “Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,” alisema Batuli.

Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve
kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za
kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
“Steve anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa
kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa
nikisikia maneno na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua
hafai,” alisema Batuli na kuongeza:“Ananiambia mimi ni msanii mchanga
ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi na nne na mwaka 2,000
wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili apate kula kwanza
nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na wasanii wa Bongo
Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na
kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:“Sipendwi na watu na sijui nini
tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye
kazi na huyu kumuacha,
yule (Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere na kuongeza:
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi nilishachezesha msanii mwengine.”

CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment