Dar es Salaam.
Baada ya kuiondoa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Kagame, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limesema litaijadili na kisha kuichukulia hatua kali klabu hiyo.
Baada ya kuiondoa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Kagame, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limesema litaijadili na kisha kuichukulia hatua kali klabu hiyo.
Wiki iliyopita, Cecafa iliiondoa Yanga kwenye michuano hiyo inayoendelea Kigali, Rwanda.
Baraza hilo lilichukua hatua hiyo kwa kile
ilichodai, Yanga ilivunja kanuni za mashindano kwa kuwasilisha majina ya
kikosi cha timu ya vijana (Yanga B) badala ya timu ya wakubwa.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema
jana: “Hatuwezi kuruhusu tabia kama hizi ziendelee, Yanga imekuwa
ikituvuruga kila mara na hii imekuwa ikitushushia heshima.
“Yanga itajadiliwa kwenye mkutano wetu ujao na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.”
Alisema klabu hiyo mara kwa mara imekuwa na utamaduni kama huo ikiwamo kugoma kucheza.
“Hii siyo mara ya kwanza, miaka minne iliyopita ilikataa kucheza na Simba na mwaka uliopita ilikataa kushiriki mashindano haya Darfur,” alisema Musonye.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu alipotafutwa kwa
simu kuzungumzia uamuzi wa Cecafa wa kuijadili na kuichukulia hatua,
alisema: “Leo ni siku ya mapumziko, siwezi kusema lolote...niko
mapumziko.”
Naye katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela alipoulizwa kuhusuana na uamuzi wa Cecafa alisema:
“Kwa mtazamo wangu, Cecafa haina mamlaka ya
kuzipatia timu aina ya wachezaji inaowataka, isipokuwa kanuni inataka
mchezaji lazima awe na leseni ya kucheza ligi ya nchi husika.”
Aliongeza: “Isitoshe Yanga ilikuwa na wachezaji
sita waliopandishwa kutoka timu B hadi timu ya wakubwa, pia tumekuwa
tukipiga kelele vijana wapewe nafasi sasa hapo kuna ubaya gani?
Inawezekana waliona mashindano ya Kagame
hayatakuwa na mvuto kwao kama Yanga ingepeleka wachezaji ambao hawana
majina makubwa kama wanayoyafahamu.”
No comments:
Post a Comment