Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
RASMI wanachama wa klabu ya Simba
sc wapatao 680 wamelazimika kuwafuta uanachama wanachama wenzao 72
waliokwenda mahakamani akiwemo mgombea aliyeenguliwa katika uchaguzi
uliopita, ‘Kidume’ Michael Richard Wambura.
Maamuzi hayo yemefikiwa katika
mkutano mkuu wa kawaida wa klabu ya Simba uliofanyika leo katika ukumbi
wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam.
Mbali na wanachama kujadili
masuala muhimu na kupokea taarifa mbalimbali za klabu katika mkutano
huo, Agenda ya wanachama 72 waliokwenda mahakamani ndio ilibebea uzito
wa juu zaidi na kila mtu alikuwa na hamu ya kutaka kujua nini hatima ya
Wambura na wenzake.
Wambura aliipeleka Simba
mahakamani mwaka 2010 na suala hilo lilisababisha kuenguliwa kwa jina
lake katika uchaguzi mkuu wa Simba na kamati ya uchaguzi chini ya
mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
Lakini alikata rufani katika
kamati ya Rufani ya shirikisho la soka Tanzania TFF, chini ya mwenyekiti
wake, Jaji Julius Mutabazi Lugaziya na kushinda, hivyo kurejeshwa
kwenye mchakato.
Sababu kubwa kumrudisha ilikuwa ni
kwamba, tangu Simba itangaze kumsimamisha uanachama Wambura mwaka 2010,
ilimuacha huru na kuendelea kushiriki shughuli za klabu kama mwanachama
hai ikiwemo kulipia ada ya kadi yake ya uanachama.
Lakini kamati ya Ndumbaro ilimuengua tena kwasababu ya kupiga kampeni kabla ya muda.
Kutokana na nguvu kubwa aliyonayo Wambura,watu walisubiri kujua nini itakuwa hatima yake leo hii.
Michael Richard Wambura amefukuzwa uanachama TFF
Mtandao huu umezungumza na makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye amethibitisha kufutwa
uanachama wanachama 72 pamoja na Wambura.
“Kikao kilikuwa kizuri na
kimeendeshwa na Rais wetu Bwana Evans Aveva. Wanachama wamepata nafasi
ya kujadili masuala ya msingi na wamepokea taarifa mbalimbali, lakini
vilevile kuna maamuzi ambayo yalifanyika,” alisema Kaburu.
“Kulikuwa na agenda kubwa ambayo ilibeba uzito mkubwa sana katika kikao cha leo ni ile ya wanachama 71 waliokwenda mahakamani.
“Ikimbukwe kuwa mwaka 2010, Bwana
Michael Richard Wambura na Bwana Nchemi walikwenda mahakamani na hadi
sasa walikuwa hawajawi kuzungumza kwenye mkutano mkuu.”
“Vilevile katika mkutano mkuu wa
2014, kuna wanachama 70 waliokwenda mahakamani kuhusu masuala ya
uchaguzi, kwahiyo leo kwa kauli moja wanachama wa klabu ya Simba wapatao
680 waliohudhuria kikao wamelaizimika kuwafuta wanachama hao
waliokwenda mahakamani”
“Kitendo walichofanya ni utovu wa
nidhamu, kwa mujibu wa katiba ya klabu yetu ya Simba, ibara ya 55
inasema mwanachama anayekwenda mahakamani basi afutwe uanachama wake”
No comments:
Post a Comment