Joyce
Kalinga Mshiriki wa Shindano la TMT ambae apia alikua mshindi kutoka
Kanda ya Kati Mkoani Dodoma akitoa maneno yake ya shukrani na pia
kuwashukuru wadau, Kampuni ya Proin Promotions na watazamaji na
waliompigia kura japokuwa bahati haikuwa yake kutokana na kutolewa
kwenye kinyanganyiro hicho baada na uchache wa kura kutoka kwa
watazamaji.
Lulu
na Joti wakitoa maelekezo kwa washiriki wawili wa Shindano la TMT ambao
waliweza kutolewa katika kinyanganyiro hiko kutokana na kupata kura
chache kutoka kwa watazamaji wa Kipindi cha TMT kinachorushwa Kila
Jumamosi saa Nne usiku.
Waendeshaji wa Show ya
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa steji,
tayari kwa kuendelea na show hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa
Mkaumbusho ya Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Mshiriki Ally Kiwendo
ambae alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu kutoka kanda ya Kusini
mkoani Mtwara akitoa maneno ya shukrani kwa Kampuni ya Proin Promoitons
ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya
kutangazwa kuaga shindano hilo kutokana na Kura kuwa chache, huku pia
akiwashukuru watazamaji na wote waliompigia kura.
Baadhi
ya washiriki wakiwa na nyuso za simanzi kutokana na Washiriki wenzao
wawili kuaga mashindano hayo.Picha zote na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo
mwisho wa Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT
ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali
kubwa.
Shindano la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za
washiriki pamoja na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho
kimejizolea umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake
ambapo awali shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili
ya kusaka vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea
katika kanda nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila
kanda waliweza Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki
ishirini kutokana kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam,
Mwishoni mwa Mwezi wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa
mafunzo na Mwalimu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona
Mwakalinga akisaidia na Mwl Issa.
Washiriki Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi
ambazo ziliweza kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka
darasani na hatimaye kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku
wakisaidiana na majaji wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy
Sarungi, Vyonne Cherry na SIngle Mtambalike.
Mpaka sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na
kupelekea kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu
wanatakiwa kutoka na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia
fainali sasa ya kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja
atajinyakulia siku ya Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi
wa 8.
Ili kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia
Kura kwa wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT"
acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00
halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae
kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.
Washiriki Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50
watakuwa chini ya Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa
filamu za Kitanzania ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na
waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na
kubwa Tanzania na la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati
No comments:
Post a Comment