MFUKO wa Dunia Global Fund, mzunguko wa 9 umesaidia Wizaya ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kutoa mabasi 6 kwa ajili ya matumizi ya vyuo mbalimbali vya uuguzi nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara, Charles Pallangyo amewakabidhi wakuu wa vyuo hivyo leo katika ofisi ya wizara iliyopo Posta, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vyuo vilivyopewa mabasi hayo ni pamoja na Chuo cha Uuguzi Bagamoyo, Tanga, Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) na vinginevyo.
Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari, Pallangyo alisema: ’’Lengo kuu ni kuongeza uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya afya, ikiwa ni pamoja na matumizi ya wanafunzi wa uuguzi katika ziara mbalimbali za kimasomo.Kikubwa ni wakuu wa vyuo kuhakikisha mabasi hayo wanayatunza ili yadumu.”
Habari/Picha na Gabriel Ng’osha/GPL
No comments:
Post a Comment