Kikosi cha yanga.
Na Wilbert Molandi
MABOSI wa Yanga, jana usiku walivamia kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji wao wanaotarajiwa kupambana na watani wao wa jadi, Simba leo Jumamosi.
MABOSI wa Yanga, jana usiku walivamia kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji wao wanaotarajiwa kupambana na watani wao wa jadi, Simba leo Jumamosi.
Timu hiyo imeweka kambi yake ya pamoja kujiandaa na mchezo huo wa
Ligi Kuu Bara kwenye Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini Dar
es Salaam.Mchezo huo unaovuta hisia za mashabiki wa soka, unatarajiwa
kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku kila moja
ikiingia uwanjani ikiwa na kocha wake mpya, Simba ni Mzambia, Patrick
Phiri na Yanga Mbrazili, Marcio Maximo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha uhakika, mabosi hao walitarajiwa
kuitembelea kambi hiyo saa 2:00 usiku kwa ajili ya kuwapa morali na
matumaini wachezaji hao.Kilisema kuwa, kikao hicho kinaendana na chakula
cha usiku kitakachowahusisha mabosi hao, wachezaji na benchi la ufundi
la timu hiyo linaloongozwa na Maximo.
Kiliongeza kuwa, pia katika kikao hicho, mabosi wanatarajiwa kutumia
nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatangazia motisha ya kiasi cha fedha kama
watafanikiwa kuwafunga Simba.
“Leo (jana) tunatarajia kutembelea kambi ya Yanga huko Mbezi Beach,
kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwapa morali wachezaji wetu wacheze
kwa bidii ili tuwafunge wapinzani wetu.
“Kikao hicho kitaenda sambamba na chakula cha usiku
kitakachoshirikisha viongozi, wachezaji na benchi zima la ufundi ili
kuwashusha hofu wachezaji wetu.
“Tunajua timu hizi zinapokutana presha inakuwa kubwa kwa wachezaji,
viongozi na mashabiki, pia tumepanga kutoa motisha kwa kuwaahidi
wachezaji wetu kama tukipata ushindi ambayo itajulikana baada ya
kukutana nao,” kilisema chanzo hicho.
No comments:
Post a Comment