MAHABAT! Kuonesha kwamba
mahaba yamemkolea, staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’
amedaiwa kukacha shughuli za muziki na kutumikia penzi lake kwa mahaba
motomoto.
Kudhihirisha hilo, chanzo chetu kimevujisha picha za mrembo huyo
akiwa na mchumba wake anayefahamika kwa jina moja la DJ Hunter wakiwa
katika malovee mazito kwa kupigana mabusu.
“Yani Snura sasa hivi muziki ameuweka pembeni anatumikia mahabati mwanzo mwisho,” kilidokeza chanzo chetu.
Jitihada za kumpata msanii huyo kuzungumzia ukimya wake kwenye gemu
hazikuzaa matunda lakini meneja wake, Mohamed Kavu ‘HK’ amekuwa
akisisitiza kuwa msanii wake huyo yupo nchini Afrika Kusini katika
shughuli za kimuziki huku pia kukiwa na madai kuwa msanii huyo ni
mjamzito tarifa ambazo pia zinakanusha na HK.
No comments:
Post a Comment