Thursday, October 23, 2014
MSHITUKO VIFO VYA WASANII
Stori: Waandishi Wetu
Misiba kila kona! Achilia mbali watu wasiokuwa na majina hasa vijana wadogo, ndani ya saa 24 wamefariki dunia wasanii wanne wa kutoka kwenye tasnia za Bongo Movies na Bongo Fleva, Amani lina habari yenye kuumiza moyo.
HAWA HAPA
Matukio hayo yalitokea kati ya Jumatatu jioni na Jumanne asubuhi ambapo kutoka kwenye tasnia ya filamu waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Sherry Salum ‘Sheri Magali’, Arafa na Benson Okumu Otieno.
Kwa upande wa Bongo Fleva, Yessaya Ambikile ‘YP’, naye alitangulia mbele ya haki ikiwa ni siku chache tu alionekana kwenye kumbi mbalimbali jijini Dar.
ALIANZA MDOGO TYSON
Jumanne jioni, gazeti hili lilipokea kwa masikitiko kifo cha mdogo wa marehemu George Okumu Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno ‘Benii’ ambaye alifariki dunia baada ya kupata homa kali na kuchanganyikiwa.
Babari za ndani zilieleza kwamba Benii alianza kuumwa mkono kawaida ambapo alitumia dawa lakini baada ya siku chache mkono huo ulianza kuvimba na kupata homa kali iliyosababisha kwenda hospitali.
Ilielezwa kwamba Benii alikwenda Hospitali ya Lugalo, Dar ambapo homa ile ilipanda kichwani na kumfanya achanganyikiwe, mwisho akaaga dunia.
Baada ya msiba huo kutokea, taratibu za kuusafirisha mwili kwenda kijijini kwao Kisumu nchini Kenya zilifanywa nyumbani kwa mdogo wake wa kike maeneo ya Sinza-White Inn jijini Dar.
Habari zilieleza kwamba Benii alikuwa akifanya kazi za uongozaji wa filamu (director) ambapo alifanikiwa kufanya filamu na wasanii mbalimbali.
Benii alianza kazi hiyo alipofika jijini Dar akiwa anaishi na kaka yake, George Tyson aliyefariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Gairo mkoani Morogoro.
“Jamani tatizo ni nini? Hata maumivu ya kifo cha kaka yake hajaisha, jamani na Benii naye? Tumuombe sana Mungu atuepushe na balaa hili la vifo,” alisema mwigizaji mkubwa Bongo, William Mtitu.
ARAFA WA BONGO MUVI AFIA INDIA!
Huku na huku, wakati watu wakitafakari kifo cha Benii na taratibu za kuusafirisha mwili wake, ghafla ziliibuka habari nyingine mbaya kuwa chipukizi wa Bongo Movies aliyetajwa kwa jina moja la Arafa naye aliaga dunia jioni hiyo ya Jumatatu.
Habari zilieleza kwamba Arafa, mtoto mzuri mwenye mvuto huku akiwa na umri chini ya miaka 20, anadaiwa kupelekwa nchini India na mama mmoja kwa shughuli binafsi.Ilielezwa kwamba, akiwa nchini humo aliumwa ghafla (ugonjwa haukutajwa) ndipo akapoteza uhai hivyo taratibu za kuurejesha mwili wake Bongo zinaendelea.
YP NAYE AAGA DUNIA
Msanii YP kutoka Kundi la TMK Wanaume Family, naye aliaga dunia usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii.
Habari kutoka kwa familia yake zilieleza kwamba YP alianza kusumbuliwa na kifua tangu mwezi Machi, mwaka huu ambapo alitibiwa na kuanza dozi.
Kwa mujibu wa mkewe, Sakina Robert na dada yake Hawa Ambikile, YP alimaliza dozi mwezi Septemba, mwaka huu ambapo hivi karibuni hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi.Mkewe alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Temeke, Dar ambako alipatiwa matibabu hadi umauti.
Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fela alisema msiba wa msanii huyo uliwekwa Keko, Dar nyumbani kwa baba yake na alitarajiwa kuzikwa jana saa 10:00 jioni kwenye Makaburi ya Chang’ombe jijini Dar.
Fela alisema kuwa YP alifanya vizuri kimuziki wakati na msanii mwingine Y Dash ambapo alisikika kwenye ngoma kibao kama Ulipenda Pesa na Pumzika.
MASKINI! ALIPANGA KUACHIA NGOMA MPYA
Ngoma nyingine nyingi alifanya na TMK Wanaume Family kama Twende Zetu ya Chegge Chigunda, Dar Mpaka Moro, Kichwa Kinauma na Tufurahi na tayari alikuwa amerekodi wimbo wake mpya akiwashirikisha Tip Top Connection unaokwenda kwa jina la Wazee wa Jiji aliopanga kuuachia mwezi ujao.
YP ameacha mke na mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka saba.
BURIANI SHERRY MAGALI!
Wakati pigo la TMK Wanaume Family likiumiza, majira ya saa 6:00 mchana, siku ya Jumanne iliyopita, ghafla kuliibuka habari nyingine mbaya kwenye Bongo Movies baada ya kuondokewa na mwigizaji ambaye ni mchekeshaji, Sherry Magali.
Sherry Magali aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kifua na moyo kwa muda mrefu.
Jumamosi iliyopita mwanahabari wetu alimtembelea wodi namba nane ambapo Sherry Magali alisimulia namna alivyokuwa akipata maumivi makali nay a muda mrefu tangu mwaka jana huku akionekana kudhoofu mwili na kukosa nguvu.
Baada ya kukutwa na umauti, msiba uliwekwa nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa kwa mzee Msafiri Ngedele.
Mazishi ya Sherry yalitarajiwa kufanyika jana kwenye makaburi ya Kola mjini hapa.
Enzi za uzima wake, Sherry Magali alisifika kwa kuchekesha na lile umbo lake zuri lililokuwa likiwatoa midume udenda.Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi-Mhariri.
Imeandaliwa na Hamida Hassan, Chande Abdallah, Deogratius Mongela, Shani Ramadhan, Gladness Mallya na Dustan Shekidele, Morogoro.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment