Kwa mujibu wa chanzo makini, jamaa huyo alikuwa na mwenzie ambaye inadaiwa kuwa ni kabila moja kwenye gari ambapo aliposimama maeneo hayo aliwaambia watu kuwa mwenzake huyo alikuwa amelewa baada ya kufakamia pombe za ofa.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mwenzake huyo baada ya kuona swaiba wake hajitambui, aliamua kumshusha maeneo hayo na kumlaza chini kisha kumuwekea karatasi kifuani iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka; “for sale”.
Chanzo kiliendelea kuweka wazi kuwa mtu
huyo alianza kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo kuwa
kama kuna mtu ana shida na ‘mtoto’ anapatikana kwa bei ya maelewano huku
akiwakataza kumpepea.
“Jamaa alizuia watu wasimpepee akidai kuwa amejitakia kwani
haiwezekani mtu upige masanga kiasi cha kutojitambua,” kilisema chanzo
hicho.Mapaparazi wetu walifika eneo la tukio na kujionea baadhi ya vijana wa mjini wakitaka kumfanyia kitu mbaya lakini kuna mzee mmoja aliwazuia.
No comments:
Post a Comment