Na Waandishi wetu/Risasi
HALI ni tete! Wazazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim na Abdul Juma wako hoi vitandani wakikabiliwa na maradhi mbalimbali, Risasi Jumamosi lina taarifa kamili.
MAMA DIAMONDHALI ni tete! Wazazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim na Abdul Juma wako hoi vitandani wakikabiliwa na maradhi mbalimbali, Risasi Jumamosi lina taarifa kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, mama Diamond hajiwezi kwa mwezi mmoja sasa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza sehemu ya mwili na kushindwa kutembea. Anaugulia nyumbani kwake, Sinza ya Mori jijini Dar es Salaam.
YADAIWA KUWA SIRI
Habari zinadai kuwa, ugonjwa wa mama huyo umefanywa kuwa siri kwa watu wengine lakini bila kujulikana kisa cha usiri huo.
BABA DIAMOND
Chanzo hicho kilieleza kuwa, baba Diamond kwa muda mrefu usiorekodiwa siku, anasumbuliwa na maumivu makali ya miguu, naye kwa kiasi cha kushindwa kutembea.
“Yeye anaugulia mafichoni kwani ndugu zake wamemficha mahali pasipojulikana ili watu wasimwone. Inaaminika kuna mambo ya kishirikina ndani yake,” kilisema chanzo hicho bila kufafanua ushirikina wa vipi!
RISASI LATAKA UTHIBITISHO
Ili kupata mzani sawa wa madai hayo, Risasi Jumamosi liliingia mtaani kwa wahusika wote.
Ili kupata mzani sawa wa madai hayo, Risasi Jumamosi liliingia mtaani kwa wahusika wote.
BREKI YA KWANZA
Katikati ya wiki hii, Risasi Jumamosi lilifika nyumbani kwa mama Diamond na kugonga geti kubwa. Msichana mmoja alitoka na kufungua geti.
Msichana: “Nikusaidie nini?”
Risasi Jumamosi: “Nimekuja kumwona mama Diamond, nasikia anaumwa sana.”
Msichana: (anafikiri kwa muda). “Mh! Ngoja nikuitie mtu mmoja uongee naye.”
Baada ya dakika mbili,mwanamke mmoja alifika getini na kukutana uso kwa uso na Risasi Jumamosi, ikawa hivi:
Mwanamke: “Eti unasemaje?”
Risasi Jumamosi: “Nimekuja kumjulia hali mama Diamond, tumesikia anaumwa.”
Mwanamke: (naye anafikiria kwa muda). “Hebu subiri kwanza.” (akaondoka).
BAADA YA DAKIKA MBILI TENA
Baada ya dakika mbili, msichana wa kwanza ndiye aliyerudi getini na kusema:
“Mama Diamond mbona hayupo, alitoka. Ni mzima na ameenda kwenye shughuli zake kama kawaida.”

MASWALI
Risasi Jumamosi liliondoka na maswali kuhusu majibu ya msichana huyo.
Kama kweli haumwi na alikwenda kwenye shughuli zake kama kawaida, kwa nini jibu hilo lisipatikane awali? Kulikuwa na ulazima gani kwa msichana huyo kutojibu ametoka mpaka akaenda kumwita mwanamke ambaye naye alishindwa kusema na kurudi ndani kumtuma msichana huyo? Sababu wanayo wenyewe!
DAKTARI ASHAURI
Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa viungo, alishauri kuwa endapo mama Diamond amepooza ni vyema akapata tiba kwa wataalamu wa viungo mapema kwani tatizo linaweza kuongezeka.
BABA DIAMOND SASA
Risasi Jumamosi lilifunga safari hadi Magomeni ya Kagera, Dar ambako ni nyumbani kwa Baba Diamond.
Baada ya kugonga mlango, mwanamke mmoja alitoka. Baada ya Risasi Jumamosi kujieleza naye alijitambulisha kuwa ndiye mke wa sasa wa baba Diamond.
Risasi Jumamosi: “Tumesikia mzee Abdul, baba yake Diamond anaumwa sana. sasa nimekuja kumjulia hali.”
Mke: “Ni kweli Abdul anaumwa, anasumbuliwa na miguu lakini haugulii hapa.”
Risasi Jumamosi: “Anaugulia wapi? Kwani amelazwa?”
Mke: “Hajalazwa na anakougulia kwa kweli siwezi kupataja.”
WAPIGIWA SIMURisasi Jumamosi liliondoka na maswali kuhusu majibu ya msichana huyo.

Juzi, Risasi Jumamosi liliwasaka wazazi hao kwa njia ya simu ili kuwasikia wanasemaje kuhusu madai ya kuumwa kwao.
Mama Diamond hakupatikana hewani, lakini baba Diamond alipopatikana alisema:
“Ni kweli naumwa bwana. Miguu inasumbua sana. Si unajua hili ni tatizo langu tangu mwaka jana?”
Risasi Jumamosi: “Nakumbuka. Sasa uko wapi nije kukupa pole?”
Baba Diamond: “Asante, usiwe na wasiwasi we endelea na shughuli zako tu, ila niombee maana kidogo hali inaanza kuonesha matumaini.”
Risasi Jumamosi: “Vipi Diamond ameshafika kukuona?
Baba Diamond: “Ah! Hapana, ila mdogo wake Mwajuma (Queen Darleen). Lakini Nasibu (Diamond) sijamwona.”
Risasi Jumamosi: “Pole sana, labda ana mambo mengi kwa sasa. Basi pole sana mzee wangu.”
Baba Diamond: “Haya nashukuru sana.”
DIAMOND MACHOZI TUPU
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na staa huyo, kutokana na hali aliyonayo mama yake, amekuwa akilia mwenyewe pindi akiwaza hatma ya mama yake ingawa simu yake alipopigiwa na mwanahabari wetu, hakupokea.
No comments:
Post a Comment