Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Hellen
Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu changamoto za
utekelezaji wa sheria ya kura ya maoni ya Katiba. Kulia ni Mratibu wa
Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Ezekiel
Massanja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
Wapiga picha na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema
kina wasiwasi na mchakato wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika kwa
sabau ya muda mdogo ulibaki ikizingatiwa daftari la wapigakura
halijafanyiwa marekebisho pia watanzania wengi hawana uelewa na katiba
iliyopendekezwa.Kituo kimetoa mapendokezo kwa Serikali kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya maoni kwa kile kilichodaiwa katiba inayopendekezwa inamapungufu na yasiporekebishwa muda huu yanaweza kuathiri kura ya maoni na kuwakosesha watanzania wengi kushiriki haki yao kikatiba.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, DK. Hellen Kijo- Bisimba alisema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kufuatilia mchakato wa katiba, kubaini mapugufu mengi likiwemo la muda mdogo na wananchi wengi kutoelewa vizuri katiba inayopendekezwa.
"Mchakato wa kura ya maoni unaenda kukamilika Februari 28 kwa mjibu wa sheria ya kura hiyo.Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga kura ndipo kura ipigwe, ukizingatia zimebaki siku takribani 25 kufikiaki hitimisho,sisi tunaona kuna changamoto ya muda na ni vyema zoezi hilo lisongezwe mbele,"alisema.
Aliongeza kuwa vifaa vya BRV vinavyotarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza na tume ya uchaguzi vimeonesha changamoto katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na hivyo kituo hicho kinawasiwasi na mchakato mzima wa upatikaji wa katiba iliyo bora.
"Kifungu cha 10 katika katiba inayopendekezwa kimezungumzia vituo vya kupigia kura, kwamba vitapangwa kulingana na maeneo yaliyo na watu wengi katika maeneo husika wasiwasi wangu hapa tume inaweza kutotumia majimbo ya zamani na kutengeza majimbo mpya,"alisema.
Bisimba alisema changamoto nyingine katika mchakatio huo ni Usajili wa kamati za kura ya maoni katika kuikubali au kuikataa kura hiyo katiba inaelekeza kamati ni lazima ipeleke maombi kabla ya siku 21 kupigwa kwa kura ya maoni.
"Utaratibu ambao sisi kulingana na uzoefu wetu wa kufanya kazi tunaona haya ni masharti magumu yanayoekekezwa kwenye kamati za kura, kwani inawataka pia kueleza vyanzo vya mapato yao kitu ambacho kinaweza kusababisha kamati zingine kutopata usajili,"alisema.
Dk.Bisimba aliongeza kuwa changamoto ambayo kituo kinaona kuwa ni kiini macho ni pale inapoelezwa kwamba wanzazibar waishio Tanzania bara wakipiga kura kura zao zitahesambiwa upande wa zanzibar.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment