Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
Mama na mwana wakiwa ni wenye furaha baada ya kukutana tena.
“Mama amerejea juzikati kutoka kwenye matibabu nchini India alikokuwa
amepelekwa, hivyo tunamshukuru Mungu sasa anaendelea vizuri na afya
yake kwa jumla inaridhisha ingawa ana programu ya kufanya mazoezi mepesi
ili aweze kuimarika zaidi ya vile alivyokuwa awali.“Pia kuna dawa ambazo alipewa kwa ajili ya kumpatia nguvu zaidi,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa ombi la kutotajwa gazetini.
Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa mama Diamond ambapo lilihakikishiwa kwamba bimkubwa huyo alikuwa ndani amelala na Diamond yupo nchini Afrika Kusini kikazi.
No comments:
Post a Comment