Vitu vikiwa nje baada ya nyumba kuvunjwa.
Mabaunsa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo usiku wa kuamkia Februari
24, mwaka huu wakati wanafamilia hao pamoja na wapangaji wawili wakiwa
wamelala ndani ya nyumba hiyo.Chanzo makini kimeeleza kuwa, mabaunsa hao walipofika kwenye nyumba hiyo, waliamuru watu wote waliokuwa ndani watoke nje wakidai wamepewa maagizo ya kuvunja nyumba hiyo na jamaa mmoja (jina tunalihifadhi kwa sasa).
Mabaunsa hao walianza kubomoa kuta za nyumba hiyo bila kujali watoto na wapangaji kama wametoka nje au la ambapo hali hiyo ilisababisha usumbufu na upotevu wa baadhi ya vitu ambavyo thamani yake haikupatikana mara moja.
Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa familia hiyo, Edwin Lyimo, baba yake anamiliki eneo hilo kihalali tangu mwaka 1977 kwa namba ya kiwanja Block C Namba 68, Namba ya Hati 21818 yenye jina la usajili, Wilson Fataeli Lyimo.
Edwin aliendelea kufunguka kuwa, awali familia hiyo ilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao kuhusu kiwanja na nyumba hiyo hadi kufikishana Mahakama ya Ardhi lakini ghafla wameshangaa kuona mabaunsa hao wamekuja kuvunja nyumba hiyo.
Waandishi wetu walifika eneo la tukio na kukuta nyumba ya familia hiyo ikiwa imebomolewa huku wenyewe wakiweka mahema ili kujisitiri na mvua na jua huku wakiwa hawana msaada wowote.
Jitihada za kumpata jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao ili aweze kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana hewani, jitihada zinaendelea.
No comments:
Post a Comment