EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, June 4, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAR 4/6/2013

11 cfaf210 164808 7ac7f

Nec yapendekezwa kuvunjwa, iundwe tume huru.

Dar es Salaam. 
Rasimu ya Katiba Mpya iliyozinduliwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, imependekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ivunjwe na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi.

 Jaji Warioba alisema Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajumbe ambao watateuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge, baada ya kutuma maombi na kufanyiwa usaili. 
Jaji Warioba alisema muundo wa tume hiyo mpya, utahusisha kufutwa kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo sehemu ya majukumu yake, yatapelekwa kwenye tume hiyo. 

 Alitaja sifa za wajumbe hiyo kuwa, mwombaji kutokuwa mwanasiasa, mwanaharakati au kutotokana na taasisi yoyote ya kiraia. “Majina ya waombaji yatachambuliwa na kamati ya uteuzi ambayo mwenyekiti wake atakuwa ni Jaji mkuu na viongozi wengine sita, ambao ni majaji wakuu wa nchi washirika, 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, maspika wa Bunge wa nchi washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu,” alisema Jaji Warioba. Jaji Warioba alisema baada ya kamati hiyo kupendekeza majina matatu yanayofaa, yatawasilishwa kwa Rais ambaye atateua mwenyekiti, makamu na wajumbe wengine, kabla majina hayo hayajapelekwa bungeni kwa ajili ya uthibitisho. 

Licha ya hilo, Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na mamlaka ya kupokea pingamizi za matokeo ya uchaguzi wa urais ndani ya kipindi ya mwezi mmoja baada ya kutangazwa. Kwa mujibu wa Katiba ya sasa, Mwenyekiti wa tume hiyo amekuwa akiteuliwa moja kwa moja na Rais bila kuhojiwa au kujadiliwa na Bunge au kamati yoyote.

M2 THE P ANA USHAHIDI WOTE KATIKA KIFO CHA ALBERT MANGWEA.

Na Mwandishi Wetu
MBIVU na mbichi sasa zinaweza kujulikana, kinachoombwa ni muda tu, kwani mng’amuzi halisi kuhusu kifo tata cha mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’, yupo kwenye mazingira mazuri kueleza kilichotokea.

KWA NINI ANA USHAHIDI WOTE?
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya mwisho nchini Afrika Kusini.
M2 The P, alipatwa na matatizo sawa na marehemu Ngwea, isipokuwa mwenzake ilifikia hatua mbaya na kupoteza maisha huku yeye akibaki mahututi kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya St. Helen Joseph, jijini Johannesburg nchini humo.
Jambo la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo  alipokwenda kwenye shughuli zake.

JAWABU LA SUMU 
Moja ya mambo yanayozungumzwa pembeni ni kwamba kuna uwezekano mkubwa marehemu Ngwea na M2 The P  waliwekewa sumu kwenye chakula au kupuliziwa ‘laivu’ kisha kutokea yaliyotokea, lengo likiwa kuwadhulumu mzigo wa fedha nyingi waliokuwa nao, hivyo kupona kwa mmoja huyo ni matakwa ya Mungu ili awe shahidi namba moja wa kifo cha Ngwea.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu jamani, M2 The P anaendelea vizuri sana, kwa sasa anazungumza. Naamini yeye amepona kwa ajili ya kufichua kilichofichika nyuma ya kifo cha mwenzake.
“Kama kweli walilishwa sumu kwenye chakula au walipuliziwa au lolote lile lingine, M2 The P anajua kila kitu kwani walikuwa wote kwa siku nzima mpaka wanarudi nyumbani alfajiri kwa safari ya kurudi Bongo.

Mwili wa Ngwair leo mchana

SHIRIKISHO la Muziki Tanzania, limesema kuwa mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea ‘Ngwair’, sasa unatarajiwa kuwasili leo mchana.

Mwili wa msanii huyo aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini, umekuwa ukipigwa danadana ujio wake, kila ulipotangazwa.

Rais wa Shirikisho hilo, Ado Novemba, alisema kwamba mwili huo unatarajiwa kuwasili leo majira ya saa nane mchana.

Alisema kwa sasa kila kitu kiko tayari, hivyo mwili ukifika utaagwa siku utakayofika na baadaye atakwenda kuzikwa nyumbani kwao Kihonda mkoani Morogoro.
Ngwair, alizaliwa 1982 na nyota yake ilianza kuchomoza katika kundi la East Zoo mkoani Dodoma.

Viti Maalumu vyafutwa, ubunge kuwa na ukomo

Dar es Salaam. 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya Katiba Mpya ukomo wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu bungeni.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema jana, wanapendekeza kwamba ubunge uwe na ukomo wa vipindi vitatu vya miaka mitano, mitano akimaanisha kwamba kipindi cha mtu kuwa mbunge hakiwezi kuvuka miaka 15.

Rasimu hiyo ya Katiba imependekeza kutokuwapo tena kwa Viti Maalumu na badala yake, imetaka kuwapo kwa nafasi tano za uteuzi zibaki kwa Rais ambazo zitahusisha makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pekee.


Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75.

Mwenyekiti huyo alisema, wananchi watakuwa na mamlaka ya kumwondoa madarakani mbunge wao endapo hawataridhishwa na utendaji kazi wake.
Alisema hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa wabunge kwa wabunge watakaopitia kwenye vyama vya siasa na badala yake jimbo litakapokuwa wazi chama kilichokuwa kikiongoza kitateua atakayeshika wadhifa huo.

“Uchaguzi mdogo utafanyika pindi tu aliyekuwa akiongoza alitokana na mgombea huru (binafsi) hivyo, Tume huru ya Uchaguzi itatakiwa kuandaa uchaguzi mdogo,” alisema Jaji Warioba.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba jana ilizindua rasimu ya Katiba Mpya -Tanzania mpya.

Dar es Salaam. 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba jana ilizindua rasimu ya Katiba Mpya inayopendekeza kuwapo kwa mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa utawala, yakiwamo ya kuwa na Serikali Tatu; Shirikisho la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar.


Mabadiliko mengine yaliyosheheni kwenye rasimu hiyo ni kufutwa kwa viti maalumu vya ubunge, suala la maadili ya viongozi wa taifa, umri wa urais kubaki kama ulivyokuwa na kuruhusiwa kwa wagombea binafsi katika ngazi zote; urais, ubunge, udiwani mpaka ngazi za mitaa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema Tume pia imependekeza kuingizwa kwenye Katiba Mpya mambo kadhaa kama Tunu, Dira na Misingi ya Taifa.

“Tulitaka kuifanya rasimu hii iwe fupi kadri iwezekanavyo, lakini kutokana na wingi wa maoni tumeifanya iwe na Ibara 240. Katiba ya sasa ina Ibara 152,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:

“Tumeendelea kuitambua misingi mikuu minne ya taifa ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Lakini pia tukaongeza misingi mingine mitatu ambayo ni Usawa, Umoja na Mshikamano. Tumependekeza Katiba yetu mpya iwe na misingi saba.”
Jaji Warioba alisema Tume pia imetambua mambo kadhaa kuwa ni Tunu za Taifa: “Tunu ya kwanza ni Utu. Tunaamini kuwa watu wote ni sawa, tusiwe na ubaguzi wala tofauti zozote. 

Tunu nyingine ni Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi Uwajibikaji na Lugha ya Kiswahili.”
Jaji Warioba alisema pia kuwa Tume imebainisha malengo ya Taifa ambayo yatakuwa mwongozo wa Mihimili ya Dola; Serikali, Bunge na Mahakama.

“Malengo hayo yatakuwa ya aina mbalimbali. Kuna malengo ya kisiasa, kiuchumi, kimazingira na mengine mengi yatakayofafanuliwa baadaye,” alisema.
Jaji Warioba alisema Tume pia imependekeza Katiba ijayo ionyeshe wazi maadili ya kijamii, kiutawala na kiuongozi.

Che Mundugwao kortini kwa wizi wa pasipoti 26

 
MSANII mahiri wa muziki wa asili nchini, Chigwele Che Mundugwao (46), na wenzake watatu jana walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la wizi wa pasipoti 26.

Che Mundugwao anashtakiwa na wenzake, Ofisa Manunuzi wa Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kilwasha (31), Mhandisi wa Idara ya Zimamoto na Uokoaji, Kenneth Pius (37), na mfanyabiashara, Ally Jabir (34).

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Ladislaus Komanya, mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana, alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 384 cha Sheria ya Kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.

Wakili Komanya alieleza kuwa kati ya Aprili 16 na Mei 10, mwaka huu, Shimweta akiwa ni mtumishi wa umma, makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, aliiba paspoti 26 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Komanya alidai kuwa washtakiwa Chigwele, Kenneth na Ally, Mei 30 mwaka huu huko Yombo Makangarawe jijini Dar es Salaam, walikamatwa wakiwa na pasipoti hizo 26 za wizi.
Kuhusu Che Mundugwao, wakili Komanya alidai kuwa mshtakiwa huyo Aprili 22, mwaka huu, alikamatwa akimiliki paspoti 12 za watu wengine, bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa Mei, mwaka huu, Che Mundugwao, pia alikamatwa na maofisa wa usalama akimiliki pasipoti nyingine mbili zenye majina ya watu wengine bila ya sababu yoyote ya msingi.

WADUDU NI CHAKULA BORA

Repoti mpya ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), limetoa taarifa hivi karibuni ikiwahimiza watu duniani kula wadudu kwa wingi kwani ni miongoni mwa vyakula bora, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha virutubisho bora vya mwili.
Senene.
Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba lishe. Aidha, wadudu wameelezwa kuwa ni rafiki wa mazingira na ni rahisi kuwafuga au kuwakamata.

Inakadiriwa na shirika hilo kuwa kiasi cha watu bilioni 2 duniani wanatumia wadudu kama sehemu ya milo yao ya kila siku. Imeshauriwa watu kupendelea kula wadudu kutokana na ukweli kwamba protini inayopatikana kwenye wadudu hao ni bora zaidi  kuliko ile inayopatikana kwenye nyama ya kuku, ng’ombe, nguruwe na samaki.

Mbali ya wadudu kuwa ni chanzo kikuu cha protini na mafuta mazuri kama ya samaki (fish oil), lakini pia ni chanzo kizuri cha madini ya kashiamu (calcium), chuma (iron), seleniamu (selenium), zinki (zinc) na Vitamini B.

Kumbikumbi.
WADUDU WA TANZANIA
Kuna aina zaidi ya elfu tisa ya wadudu wanaoliwa sehemu mbalimbali duniani. Lakini kwa nchini

Tanzania, kuna aina kuu mbili za wadudu ambao wanajulikana na kutumiwa kama sehemu ya kitoweo katika familia nyingi nchini, hasa vijijini.

Monday, June 3, 2013

PICHA ZA MWILI WA ALBERT MANGWEHA ULIVYOAGWA LEO NCHINI SOUTH AFRICA

Watanzania waishio nchini South Africa, wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa mwanamuziki ALBERT MANGWEA aliefia nchini humo … Hii hapa chini moja ya picha inayoonesha watu wakiaga mwili huo …
Ngwair-SA
Mwili wa Marehemu Ngwair utawasili kesho jijini Dar Es Salaam na kuagwa na fans, marafiki na ndugu katika viwanja vya leaders club, kinondoni kabla ya safari ya kwenda Morogoro, ambapo atazikwa huko karibu kabisa na kaburi la baba yake mzazi …
R.I.P Albert Mangweha.
Muda huu wa saa kumi na Mbili kwa saa za Afrika mashariki
kwa saa za South Africa ni
saa kumi na Moja jioni.....tukiwa bado tupo kwenye majonzi
makubwa yakupotelewa na ndugu yetu
Albert Mangweha.....Baada ya ratiba kupangika watanzania
waishio nchini South Africa
wamepata nafasi ya kuaga mwili wa Albert Mangweha
 kuelekea katika safari ya mwisho...wakiongozwa na Msanii
Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru
,Kinjeketile wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini South Africa

ZIFUATAZO NI PICHA 4 WATANZANIA WAISHIO SOUTH
 AFRICA WAKIAGA MWILI WA
ALBERT MANGWEHA:
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjotSQDTYDT036YkZO5FmFqhFmx_e_atGZLpy5BVGfGuYHwCja4ZOt94wvH13BwYinjwTt7c3X3mENGs_S0912uRt75nbWXSAVmZ-ww4rZHNIcqg273t399r-xOKlDODNa3FZqgLqxDbqq0/s640/IMG-20130603-WA006.jpg
Shugli ya kuaga mwili ikiendelea muda huu nchini South Africa.....

HATIMAYE CHELSEA IMESIBITISHA JOSE MOURINHO NDIYE KOCHA MPYA.

Chelsea Football Club is delighted to announce the appointment of Jose Mourinho as our new first team manager.
KOCHA MPYA WA CHELSEA JOSE MOURINHO AMERUDI TENA KUNAKO CLABU HIYO.

RASIMU YA KATIBA YAZINDULIWA LEO NA HAYA NI MACHACHE YALIOMO.

ACHE YALIOMO!

Rasimu ya Katiba mpya leo imeziduliwa rasimi jijini Dar es salaam ambapo viongozi mbalimbali wameudhulia katika uziduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya karimjee na haya ni mtasali tu wa yale yaliopendekezwa kuwemo kwenye Katiba Mpya.

-SPIKA NA NAIBU WAKE WASIWE WABUNGE,WALA WASIWE VIONGOZI WA SIASA. 
 -  UWEPO MUUNDO WA SERIKALI TATU.
  - MAWAZIRI WASIZIDI KUMI NA TANO (15)
  - TUME YA UCHAGUZI IJULIKANE KAMA TUME UHURU YA UCHAGUZI.
    -KUSIWE NA UCHAGUZI MDOGO. 
-KIKOMO CHA KUWA MBUNGE KIWE MIAKA MITATU (3)
 -KATIBU MKUU KIONGOZI KUSIBITISHWA NA BUNGE.
 - MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI WASIBITISHWE NA BUNGE MARA RAIS ANAPOWATEUA.
 -MATOKEO YA URAIS YALUHUSIWE KUOJIWA MAHAKAMANI KAMA MTU -ASIPOLIZIKA NDANI YA MWEZI MMOJA MAHAKAMA KUU.
    -MGOMBEA APATE ASILIMIA 50%KUTANGAZWA MSHINDI.

          KUWEPO NA MGOMBEA BINAFSI

Hayo ni baadhi tu ya yale yaliomo sasa hatua inayofata ni Mabaraza ya Katiba kukaa na kuipitia Rasimu hii na kuona kwenye mapungufu kulekebisha kaa tayari kuipata rasimu yote jinsi ilivyo mda mfupi ujao..........!!!!

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YA MAGARI IMETOKEA ENEO LA NANE NANE DARAJANI UYOLE MBEYA , YAJERUHI NA WATU WANNE WAHOFIWA KUFA

 GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE IKIWA IMEGONGANA USO KWA USO NA GARI AINA YA LAND CRUISER
 
HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA 
HIVI NDIVYO DALADALA HII ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI HIYO KUTOKEA 

TAMKO LA BALOZI WA TANZANIA WA AFRICA YA KUSINI KUHUSU KUCHELEWA KUFIKA KWA MWILI WA MAREHEMU NGWAIR TANZANIA.

Balozi wa Tanzania Africa ya Kusini Radhia Msuya.
Balozi wa Tanzania Africa ya Kusini kwenye picha hapo juu ametoa pole kwa familia,wasanii na wadau wote kwa kupotelewa na kijana ambaye bado watu walikuwa wanamuhitaji.Amesema kuwa mwili wa marehemu Ngwair umechelewa kufika Tanzania kutokana na post mortem na taratibu za kupata kibali cha kusafirisha mwili huo kutoka Serikali ya Africa ya Kusini.Radhia alisema kuwa kama taratibu zote zitaenda sawa mwili huo utawasili siku ya Jumanne Tanzania.MSIKILIZE hapo chini;Habari na Anna Peter Blog.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI TOKA KWA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO KUTOKANA NA KIFO CHA MANGWEHA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea

kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii

 wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangweha,

aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa

 katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013.

Kifo cha Albert Mangweha ni pigo kubwa kwa fani ya muziki

hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika

fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji

ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana

ndani na nje ya nchi.

Albert Mangweha atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa

 muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.

Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba

wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.

Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni

kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya

wakati wa uhai wake.

“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangweha

mahala pema peponi.”

Imetolewa na

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo

Dkt Fenella Mukangara

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate