Bodi
ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imeanza kuonyesha cheche zake kwa
kishindo, kwa kufumua mfumo mzima wa uongozi na mashindano haya makubwa na
yenye mafanikio nchini.Katika kikao chake kilichofanyika mwishoni mwa
wiki,chini ya makamu mwenye kiti wa bodi hiyo Ndugu Abubari Omari Abubakari,
bodi imechukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuboresha na kimarisha Mashindano
haya lenye manufaa makubwa kiuchumi,kitamaduni na kijamii kitaifa na kimataifa.
Bodi
imeazimia kuchukua hatua katika Nyanja mbalimbali za mashindano haya, kuanzia
mfumo wa mashindano,uongozi,utawala na uendeshaji mzima wa mashindano. Bodi
imeazimia kufanya mabadiliko haya, na kuwa Miss Tourism Tanzania Organisation,
ni taasisi ambayo kuanzia sasa itaendeshwa kwa mfumo wa kitaasisi, ambayo sasa
badala ya kuwa taasisi ya mashindano ya urembo pekee, inakuwa ni taasisi ya
kuhamasisha na kutangaza Utalii, Utamaduni,
Mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Bidhaa za Tanzania, Uvuvi,
Wanyama Pori, Madini,
Hifadhi za Bahari, sera za Taifa za Utalii, Utamaduni, Kilimo, Mazingira, Umasikini,
Vijana, Wanawake na watoto, Utalii wa Ndani,Utalii wa Kitamaduni, Utalii wa
Michezo na Utalii wa Mikutano. Pia kupiga vita Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu, Umasikini,
Maradhi, Ujinga, Tamaduni kongwe na Potifu kitaifa na kimataifa.Malengo haya
yatafikiwa kupitia mashindano ya Miss /Binti Utalii Tanzania, Miss tourism Tanzania
International, Miss Tourism University World, Miss Heritage World, Tanzania
Beauty and Model Management, National Parks Marathon, Tanzania Great Safari and
Tour na Tanzania Cultural Carnival and Festival kila mwaka.
Aidha
kuanzia mwaka huu, pamoja na Shindano la kitaifa la Miss Utalii Tanzania,
fainali za Taifa zitakwenda sambamba na Miss Tourism Tanzani International,
ambapo washiriki wa Tanzania watapanda jukwaani kuwania taji la taifa sambamba
na washiriki waalikwa kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwania taji la Miss
Tourism Tanzania International,ambapo washindi wake watakuwa mabalozi wa Tanzania
katika mabra na nchi zao. Kwa kuwa na washiriki kutoka katika mabara yote
duniani ikiwemo Ulaya,Marekani,Asia,India,Marekani Kusini,Afrika na Urusi Shindano
la Miss Utalii Tanzania sasa litakuwa ni la kimataifa na lenye uwezo mkubwa wa
kuitangaza Tanzania, Utalii ,Utamaduni na mali asili zake kimataifa, kwani
fainali za taifa kuanzia mwaka huu, zitaonyeshwa LIVE duniani kote kupitia
Televisheni na mitandao ya Internet.
Bodi pia imepitisha azimio la kutumia
lugha ya Kiswahili kwa wawakilishi wote wa mashindano haya katika mashindano ya
dunia na mengine ya kimataifa, ili kukitangaza vyema Kiswahili ambayo ni lugha
ya limataifa na ya Afrika, kama ambavyo washiriki kutoka mataifa mengine
wanavyo tumia lugha zao na kushinda mataji ya Dunia.
Bodi
imefanya uchambuzi wa kina wa wakurugenzi na waandaaji wa ngazi mbalimbali, na
kupitisha azimio la kuwataka waandaaji wa Majimbo (Vitongoji) ,Wilaya, Mikoa, Mikoa
maalum ya Vyuo Vikuu, Kanda na Kanda maalum za Vyuo Vikuu kuomba upya na kutoa
fulsa kwa watu na makampuni mbalimbali kuomba kuandaa katika ngazi yoyote
nchini, isipokuwa waandaaji wake katika mabano Dar es Salaam, Ilala na Temeke (Film
Directors Association) Katavi (KATABI CO. LTD & COUNTRY WIDE ENTERTAINMENT) Arusha na Mara (NAMAN
201O LIMITED ),Tanga ( Kambi Mbwana
Entertainment),Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam ( ERIADO POINT VIEW)
Kanda ya Kusini (MOD INTERGRATED SOLUTION AND AWARENESS) na Kanda
ya Ziwa (FANIA BEAUTY ENTERTAINMENT) ambako waandaaji wake wanabaki kama
walivyo. Ambako waandaaji wapya wanatakiwa na wazamani wanaruhusiwa
kuomba ni:
1. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya
Kaskazini, Mashariki, Mgharibi na Kati.
2. Miss Utalii Tanzania – Kanda za vyuo Vikuu
– Kaskazini, Kusini, Kati, Magharibi, Ziwa na Mashariki.
3. Miss Utalii Tanzania –Mikoa ya Dodoma,
Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Rukwa, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza, Ruvuma,
Lindi, Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Manyara, Kilimanjaro ,Iringa, Mbeya,
Njombe.
4. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu –
Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tanga, Mwanza, Kagera, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro,
Arusha na Tabora.
5. Miss Utalii Tanzania – Majimbo yote ya
Wabunge na Wilaya.
Mwisho
wa kupokea maombi ya waandaaji wapya na wa zamani ni tarehe 12 Juni 2012,
waombaji wanaweza kutuma maobi yao kupitia anuani zetu barua pepe ambazo zina patikana
katika website (www.misstourism/utaliitanzania.com, blogspoti (misstourismorganisation.blogspot.com
na mitandao yetu ya facebook, twitter na Skype (misstourismtanzania au
missutaliitanzania). Kwa mfumo huu mpya unalenga kufikisha kwa umakini na
ustadi mkubwa Shindano hili hadi ngazi za cheni kabisa za wananchi, na kufanya
kila mbunge wa jimbo , mkuu wa Wilaya, mkuu wa Mkoa na Rais wa nchi kuwa na
mabalozi wao wa Utalii kupotia mashindano haya, ambao watasaidia na kuwa na
jukumu la kuhamasisha Utalii, Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa kitamaduni,
mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Kilimo, na Mianya ya uwekezaji katika ngazi
zao , sambamba na mamlaka za umma na binafsi za ngazi hizo, huku wakitafsiri
kwa vitendo sera husika za taifa. Aidha bodia imeazimia kuimarisha umakani na
kitengo cha uchunguzi na intelijensia cha
Shindano ili kubaini njama,hujuma na
mamluki katika Shindano hili, kabla hawaja leta madhara na kuwachukulia hatua
kali ikiwemo kuwafikisha katika Vyombo vya dola.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Abubakari alisema kuwa, pamoja na sababu za kukosa
umakini na ufanisi, waandaaji hao wa ngazi za mikoa na kanda wamekuwa
wakiruhusu warembo wasio na viwango na hata vigezo kushiriki katika mashindano,
jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni na taratibu za mashindano haya, ambayo
kwa miaka mitano mfulizo yamekuwa yaki fanya vyema katika mashindano mbalimbali
ya Dunia na kimataifa. “Tumelazimika kuchukua hatua mapewa, ili kulinda hadhi
ya mashindano haya kitaifa na kimataifa. Ni mkakati wa bodi ya mashindano sasa
kuwaondoa mashindanoni washiriki wote ambao hawakidhi viwango bila kujali
mataji watakayo kuwa wametwaa katika ngazi zao. Fainali za Taifa mwaka 2012
zitafanyika mwezi Novemba 2012 ,ili kutoa fuksa kwa waandaaji wa kanda na mikoa
iliyo salia kufanya fainali zao,pia kuzingatia kalenda mpya za mashindano ya
Dunia na kimataifa.
Asante,
Abubakari
Omari Abubakari
Makamu
Mwenyekiti Bodi ya Mashindano ya Miss/ Binti Utalii Tanzania
Nakala
Rais Miss Tourism Tanzania Organisation
No comments:
Post a Comment