Na Mwandishi wetu
HEKAHEKA
ya wimbi la mastaa wa Bongo kutumika kwenye imani inayodaiwa kuwa ni ya
kishetani duniani maarufu kwa jina la Freemason a.k.a Wajenzi Huru
inazidi kuchukua nafasi kwa kasi baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwa,
staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Massawe naye ametumbukia
humo.
NI NCHINI AFRIKA KUSINI
Kwa
mujibu wa chanzo cha uhakika, Wolper ameinamisha kichwa na kumwagiwa
maji ya imani hiyo kama ishara ya kujiunga nchini Afrika Kusini, mapema
mwaka huu.
NANI SHAHIDI?
Mmoja wa marafiki wa Wolper aliliambia
gazeti hili kwamba, Wolper alishawishiwa na msanii mwingine wa kiume wa
filamu Bongo ambaye hana jina kubwa kuwa ndiye aliyempa namba za
mawasiliano za wahusika nchini Afrika Kusini.
“Wolper ameingia
Freemason na aliyemshawishi ni msanii ….(anataja jina), yeye alimwambia
akiwa huko anaona matunda yake kwani ni imani ambayo binadamu unaishi
kama peponi,” alisema rafiki huyo.
UTAJIRI WA HARAKA WATAJWA
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, tangu Wolper amejiunga na imani hiyo inayosambaa
kwa kasi nchini Tanzania amekuwa akipata mafanikio makubwa tena kwa
haraka.
“Wee kama unataka kuamini, angalia tangu mwaka huu (2012)
umeanza, Wolper mambo yanamyookea tu. Awali alikuwa akiishi eneo ambalo
halimfai kama staa, sasa amehamia Mbezi, tena kwenye jumba zuri sana,”
alisema mtoa habari huyo.
Aliendelea kuweka wazi kuwa, magari na
miradi mingine aliyonayo si ofa kutoka kwa mchumba wake aitwaye Abdallah
Mtoro ‘Dallas’ kama anavyodai mwenyewe Wolper bali ni ‘baraka’ ya
Freemason.
Akasema: “Mmekuwa mkiandika eti kanunuliwa magari na
mchumba wake, nani kasema? Ile ni kama njia ya kukwepea tu, lakini
ukweli ni kwamba Freemason ndiyo wanambeba kwa sasa.”
Akaongeza:
“Wazazi wa Wolper wapo katika wakati mgumu, mama yake amepata fununu za
mwanaye kujiunga na Freemason na ndugu wakamweka chini kumwonya kama ni
kweli ajitoe mara moja.”
KANUMBA ALIJIUNGIA NIGERIA
Hivi
karibuni, mtu mmoja aliyejitaja kuwa ni mchungaji wa kanisa moja la
kiroho jijini Dar, George Kariuki alizungumza kupitia Kituo cha Radio
Times FM na kudai kuwa marehemu Steven Kanumba alijiunga na u-Freemason
nchini Nigeria, nchi ambayo iko mbali kidogo kutoka Tanzania kuliko
ilivyo Afrika Kusini anakodaiwa kwenda Wolper.
Hata hivyo, matokeo ya
Kanumba kujiunga yalionekana, kupata mali kwa kasi ya ajabu, nyota yake
kung’ara lakini mwisho wa yote ilifika mahali imani hiyo inatajwa na
baadhi ya watu kuwa ndiyo chanzo kikuu cha kifo chake (Mungu amlaze pema
peponi-amina).
BOFYA HAPA UMSIKIE WOLPER
Baada ya madai hayo,
Risasi Jumamosi lilimsaka Wolper kwa nguvu zote na kubahatika kukutana
naye siku ya Jumatano maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baada ya salamu, msanii huyo mwenye aibu kwa mbali, alisomewa ‘mashitaka’ yake yote huku akiwa amemkazia macho paparazi.
Wolper:
“Mh! jamani, mnajua haya mambo bwana yana siri kubwa ndani yake. Wako
watu wanatajwa ni Freemason, wengine wapo lakini hawatajwi, ni kwa
nini?”
WOLPER JIBU SWALI
Paparazi: “Labda kikubwa ungetuambia ni kweli upo huko au si kweli?”
Wolper:
“Unajua bwana, mimi sina hela kama wanavyosema watu. Na haya yote
yametokana na nilivyomsaidia Sajuki (Juma Kilowoko). Yule nilimsaidia
kwa sababu niliguswa kutoka moyoni, lakini familia yangu yenyewe ina
uhitaji mkubwa sana.
“Tena naomba jamii ielewe kuwa, sina ‘minoti’ ya
kumwaga. Napata tabu watu wananifuata wakilia shida zao wakiamini nina
fedha kibao, si kweli jamani.”
WOLPER VIPI?
Paparazi: “Umezungumza vizuri, lakini hujajibu suala la kujiunga na Freemason kama ni kweli au si kweli?”
Wolper: “Mimi gari si alininunulia Dallas, mbona nilishasema jamani au?”
Paparazi: “Sawa, ulishasema, vipi kuhusu Freemason sasa?”
Wolper:
“Ni kwa sababu ya hizi nguo au? Maana nguo navaa bila kujua alama zake,
sasa kama kuna za Freemason mimi nitajuaje jamani, ee?”
HAYA SASA
“Ila
labda nikiri kitu kimoja, ni kweli niliwahi kuitwa na watu wakaniambia
nijiunge kwenye imani hiyo, waliniahidi kwamba nikikubali maisha yangu
yatakuwa mazuri na ulinzi wa afya yangu.”
Paparazi: “Ina maana hujajiunga unafikiria kwanza?”
Wolper: “We unaonaje, nijiunge au? Mimi sitaki nasikia wengi wameingia wanafanikiwa kwa kasi.”
MASWALI YA MHARIRI
Kama
kweli Wolper si Freemason, amejuaje mavazi yake yana alama ya imani
hiyo? Kwa nini anaomba ushauri huku anasema haitaki imani hiyo?
Chanzo cha habari: Risasi
Jumamosi
Kutoana na mafanikio ya ghafla ya huyu bint ukweli ni upi kati ya Freemason na Dallas?
ReplyDelete