Mke wa staa wa filamu
za Tanzania, Juma Kilowoko, Wastara Juma amesema mambo yote yanayoipata familia
yake ni mapito akiamini yatapita siku moja.
Aliyasema haya kwa
rafiki yake akizungumzia kutibiwa kwa mumewe nchini India, unafuu aliyonayo na
walivyorejea nchini.
Wastara alisema kuwa
ni vigumu kwa baadhi ya watu wasio na imani kuamini kuwa haya ni matatizo ya
kupita lakini kwake yeye anaamini yatapita na kuna siku atasimulia kwa watu
kama historia.
“Mwenyewe Wastara
anasema anaamini haya yote yanayomtokea sasa yatapita, anasema wako wasioamini
matatizo yatapita, lakini yeye anajua iko siku atayaona mambo yote ni
historia,” alisema rafiki wa Wastara alipoongea na mtandao huu.
Wastara na mumewe
Sajuki walirudi nchini hivi karibuni wakitokea nchini India ambako mwanaume
huyo alikwenda kutibiwa matatizo yake ya uvimbe tumboni.
Awali
staa huyo alitibiwa nchini Tanzania lakini hali haikubalidika ndipo harambee
ikapighwa ambapo wadau walichanga pesa na kumpeleka kutibiwa India
No comments:
Post a Comment