Mtu mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio
la mwezi uliopita katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini
Tanzania.
Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki.
Kenya inadai kuwa alivuka mpaka mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi la Al Shabab.
Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika mlipuko ambao wakuu wa Kenya wanasema ulisababishwa na bomu hilo.
Kumekuepo na sintofahamu juu ya chanzo cha
mlipuko huo- ambapo Maofisa wa Polisi walianza kwa kusema kuwa mlipuko
huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.
Mara kwa mara kundi la Al Shabab limetishia
kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Kenya kwa sababu nchi hio
ilituma vikosi nchini Somalia.
Serikali ya Kenya inalituhumu kundi la
wapiganaji wa Al Shabab kuhusiana na utekaji nyara wa watu kadhaa kwenye
ardhi yake pamoja na kusababisha hali ya wasiwasi kwenye mpaka baina
yake na Somalia.
Polisi ya Tanzania imethibitisha kwa BBC kuwa Bw.Erdogan alikamatwa na kuahidi maelezo zaidi baadaya mda mfupi.
Erdogan ni miongoni mwa watu wanne ambao Polisi ya Kenya imekua ikiwasaka tangu kutokea kwa mlipuko huo.
Ilisambaza picha yake na kuomba habari kuhusu mahali alipo.
Bw.Erdogan, anayejulikana pia kama Salahuddin
al-Kurdi, inaaminika kuwa aliwahi kusafiri kwenda Waziristan huko
Pakistan ya kaskazini magharibi mwaka 2010 ambako alijiunga na kundi la
wakereketwa wenye imani kali kabla ya kuelekea Somalia mwaka jana, kwa
mujibu wa shirika la habari Reuters.
Mapema mwaka huu, vikosi vya AU vinavyounga
mkono serikali ya mseto nchini Somalia viliongezea idadi ya askari wake
kutoka 12,000 hadi 18,000 kujumuisha vikosi vya Kenya vilivyoingia nchi
hio mnamo mwezi Oktoba mwaka jana kuwasaka wapiganaji wa Al Shabab.
Kundi la Al-Shabab, lililojiunga na mtandao wa
al-Qaeda mapema mwaka huu imefahamika lilisajili wapiganaji wa kigeni
kadhaa -wengi ambao wamewahi kupigana huko Iraq na Afghanistan.
Chanzo cha habari: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment